- Bertha Mollel, Manyara
- Wizara ya Mali asili na utalii imeikabidhi shirika la Tanapa magari makubwa 23 na mitambo 14 yenye thamani ya shilingi billion 16.455 Kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu za hifadhi nchini ikiwemo ukarabati na ujenzi wa Barabara, viwanja vya ndege vivuko madaraja na mageti ya kuingilia wageni.
- Magari na mitambo hiyo iliyotokana na mradi wa fedha za uviko (TCRP) imekabidhiwa na Waziri wa maliasili na utalii mh. Balozi Dr. pindi Chana katika hafla iliyofanyika ndani ya hifadhi ya Tarangire iliyoko mkoani Manyara.
- Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Chana alisema kuwa wizara yake imepokea Jumla ya shilingi bilioni 90.2 kuhakikisha wanaboresha miundombinu na huduma za utalii Ili kukabiliana na athari zilizojitokeza kipindi Cha ugonjwa wa uviko -19
- "Kati ya fedha hizo Tanapa wamekabidhiwa billion 45.7 Kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu za ndani ya hifadhi kuhakikisha Barabara zinapitika na kufikika mda wote bila kujali kipindi Cha masika Walavuli Wala ukame"
- Alisema kuwa katika kutekeleza maagizo hayo ya Rais Samia juu ya fedha hizo za uviko ndio maana wakanunua nyenzo hizo kusaidia utekelezaji ambapo amewataka uongozi wa Tanapa kuhakikisha wanatunza mitambo na magari hayo na yanatumika Kwa kazi kusudiwa Ili ulete tija na matunda Kwa wizara na hifadhi nchini.
- Mbali na hili Waziri Chana amewataka viongozi wa Tanapa kuhakikisha vyenzo hizo hazitumiki bila kifunga mifumo ya kielecronic ya ufuatiaji hasa ya mwendo, matumizi, na mafuta Ili kudhitibi matumizi mabaya ya nyenzo hizo.
- "lakini pia mitambo hii ni ya gharama sana, hivyo hatutapenda kuona zinaharibika haraka Kwa mda mfupi, hivyo viongozi hakikisheni madereva wanaokabidhiwa kuendesha mitambo hiyo wanapewa mafunzo ya utendaji kazi wa vifaa hivyo kabla ya kukabidhiwa na kupimwa Kwa utendaji kazi wao" alisema Waziri Chana
- Awali kamishna wa uhifadhi wa Tanapa, William Mwakilema alisema kuwa magari hayo makubwa (malori) na mitambo hiyo yenye thamani ya billion 16.455 ni miongoni mwa kiasi Cha shilingi billion 45.7 walizopokea Kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kuimarisha miundo mbinu ya hifadhi zilizoko chini ya Tanapa.
- "Fedha hizo zimetumika kununua mitambo 14, magari 23 makubwa na magari Saba madogo Kwa ajili ya kuwezesha ukarabati wa Barabara na shughuli za utalii katika hifadhi za Taifa mitambo 8 tumeshaipokea na magari makubwa 23 ambapo mitambo sita iliyosalia itapokelewa Octoba"
- Alisema magari hayo watafungwa mifumo ya kielecronic ya ufuatiliaji wa utendaji kazi wake Ili uongozi uweze kujua, magari yanakwenda wapi na yanafanya Nini Kwa Wakati Gani na yanatumia mafuta kiasi Gani yote Kwa ajili ya udhibiti Ili kuhakikisha yanaleta tija na matunda kusudiwa.
- "Tunatarajia kugawanya mitambo na magari hayo katika seti Moja kwa Kanda itakayokuwa na magari makubwa matatu, mtambo wa chain excavator Moja na compact tractor Moja na gari Moja Kwa ajili ya usimamizi na gari Moja ya kubebea mitambo"
- Alisema seti hizo watagawa Kwa Kanda za hifadhi nne ambazo ni Kwa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, itakayohdumia ziwa manyara, Arusha, Kilimanjaro na mkomazi huku Kanda ya hifadhi ya Serengeti itakuwa na seti yake, hifadhi ya Nyerere, huku Kanda ya hifadhi ya chato, itakayohidumia kisiwa Cha rubondo na zote zilizoko huko.
- Nae mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Tanapa, generali mstaafu George Waitara alisema kuwa fedha hizo zimerahisisha utendaji kazi wa bodi yake Kwa kupata nyenzo za kuboresha miundombinu za ndani ya hifadhi na huduma za utalii nchini.
- "Waziri nikuombe zinapotokea tena fursa za kifedha uipe Tanapa kipaumbele kutokana na uhitaji mkubwa ulioko lakini pia mchango wake Kwa serikali katika kukuza uchumi wa nchi"
Tags:
Utalii