Rais Samia apewa tuzo TANAPA

mwenyekiti wa bodi ya Tanapa, generali mstaafu George Waitara na akimkabidhi Waziri wa Mali asili na utalii balozi Dr.Pindi Chana tuzo ya Kuifikisha Kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kuadhimisha siku ya utalii duniani iliyofanyika kitaifa katika makao makuu ya Tanapa Arusha



BERTHA MOLLEL, ARUSHA



Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanikiwa kupewa tuzo ya utalii iliyotolewa na Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA).

Tuzo hiyo imekabidhiwa na mwenyekiti wa bodi ya Tanapa, generali mstaafu George Waitara na imepokelewa na Waziri wa Mali asili na utalii balozi Dr.Pindi Chana katika hafla ya kuadhimisha siku ya utalii duniani iliyofanyika kitaifa katika makao makuu ya Tanapa Arusha.

Akizungumzia tuzo hizo, mhifadhi mkuu wa Tanapa William Mwakilema alisema kuwa wameamua kutoa tuzo 19 Kwa wadau  ikiwa ni kutambua mchango wao katika kuhamasisha utalii nchini na kuongeza pato la Taifa.

mwenyekiti wa bodi ya Tanapa, generali mstaafu George Waitara na akimkabidhi Waziri wa Mali asili na utalii balozi Dr.Pindi Chana tuzo ya Kuifikisha Kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kuadhimisha siku ya utalii duniani iliyofanyika kitaifa katika makao makuu ya Tanapa Arusha.


"Tuzo hizi tumeanza kutoa 2019 na Leo ni za tatu ambayo tunatoa Kwa watu mbali mbali waliotoa mchango mkubwa kwenye ongezeko la utalii na mapato licha ya nchi kukumbwa na ugonjwa wa uviko ambapo wote mtakubaliana na Mimi kuwa Rais wetu anastahili kuwa namba Moja kwenye tuzo hii kutokana na mchango mkubwa hasa program ya filamu ya 'The Royal tour'

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa maliasili na utalii, balozi Dr. Chana alisema kuwa tuzo ya tatu ya Utalii zinazotolewa na Tanapa zimekuwa chachu na mafanikio makubwa ya kuhamasisha wadau kuchangamkia fursa za kukuza utalii nchini ambapo amewataka wadau hao kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuendeleza utalii nchini.

"Kwa Sasa utalii unachangia asilimia 17 ya pato la Taifa lakini mnaweza kuchangia zaidi endapo mtaweka mikakati mizuri wenye ubunifu ndani yake ya vivutio vipya zaidi"

Kwa Upande wake mwenyekiti wa bodi ya Tanapa, generali mstaafu George Waitara alisema kuwa lengo la tuzo hiyo ni kuhamasisha wadau watoe maoni na hamasa ya kufikia utekelezaji wa sera ya serikali kufikia watalii milioni tano hadi kufikia 2025.

"Pia tunalenga kufikia ukusanyaji wa Dola billion 6 Hadi kufikia 2025 hivyo watakaopata tuzo hii waendelee kutoa mchango wao na wajue waanawakilisha wengi, na waliokosa waendelee kutoa mchango wao tufikie mbali zaidi"

Wengine walipata tuzo ni Taasisi na makampuni mbali mbali za utalii ikiwemo Zara tour, wayo Afrika, Serengeti boloons safari, Afrika queen na nyinginezo
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!