Bertha Mollel, Arusha .
Wakati
matukio ya ukatili wa kijinsia yakiendelea kutia doa nchini huku Arusha
ikitajwa kuongoza mikoa mingine, baadhi ya Mashirika ya Kijamii yameungana
kuunda mtandao maalum wa kutokomeza matukio hayo yanayoacha maumivu makubwa kwa
waaathirika.
Matukio
makubwa ya ukatili yanayotajwa nchini ni pamoja na ubakaji, kulawiti, mimba za
watoto na ndoa za kulazimishwa.
kwa mujibu
wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Doroth
Gwajima, kwa mwaka 2022 pekee zaidi ya kesi 12,163 za Ukatili wa Kijinsia
yameripitiwa nchini huku waaathirika wakubwa wakiwa ni wanawake (9962) na
wanaume ni 2201.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mtandao huo jijini Arusha, mwenyekiti Rose Njilo alisema
mpango huo umeratibiwa chini ya ‘Mimutie Women Organization,’ kwa lengo
la kuzifikia jamii nyingi za pembezoni na kuwasaidia dhidi ya majanga hayo ya
ukatili wa kijinsia.
"Kesi
za unyanyasaji wa kijinsia zinatokea zaidi katika jamii za pembezoni kwa
sababu hawana taarifa sahihi za madhara ya matukio haya lakini wengi wao bado
hawajui kusoma na kuandika huku wakiwa wamefungwa chini ya Mila na desturi
zao," alieleza Bi Njilo.
Mtandao
mpya wa kupinga Ukatili wa Kijinsia unaundwa na Mimutie Women Organization
(MWO), Embuan Development Organization (EMBUDEO), Dunia Salama Foundation,
Media Aid for Indigenous and Pastoralist Community (MAIPAC), Oseremi
Development Organization na FOMA.
Njilo
alisema wakazi wa Kanda ya Kaskazini hasa Mkoa wa Arusha na Manyara wanaonekana
kukumbwa na matukio makubwa ya ukatili wa kijinsia hivyo kuhitaji elimu zaidi
ya kuripoti matukio haya, lakini pia namna ya kuepuka viatararishi na matukio
haya kutokea.
Alitaja
baadhi ya matukio ya Ukatili wa kijinsia kuwa ni unyanyasaji wa kijinsia, ndoa
za utotoni na za kulazimishwa, mashambulizi ya kikatili na kushambuliwa kwa
majeraha na wakati mwingine vifo pamoja na ukeketaji.
Njilo
alibainisha kuwa mambo mengi ya aina hiyo huwa hayaripotiwi, lakini hivi karibuni
mashirika yao yalifanikiwa kupata kesi 17 ambazo zilifikishwa mahakamani na
angalau kufanikiwa kushinda kesi moja ya kisheria zingine zikiwa katika
hatua mbalimbali za uendeshaji.
Ofisa Maendeleo
ya Jamii Mkoa wa Arusha, Blandina Nkini alisema tafiti zilizofanywa na Serikali
zimebaini kuwa matukio mengi ya Ukatili yanasababishwa na imani potofu za
kimila na malezi duni.
"Kwa
sasa tunaelekeza nguvu kwenye kutoa Elim ya malezi na makuzi bora kwa
wazazi ilii kila mmoja atambue na kutekeleza majukumu yake ambayo yataleta
watoto wenye maadili baadae watakaokuwa na hofu ya kutekeleza matukio haya ya
Ukatili"
Mwisho