![]() |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Justine
Masejo akitoa taarifa kwa wanahabari |
Arusha.
Jumla ya watu 30 mkoani Arusha wamehukumiwa kifungo cha Miaka 30 jela kila mmoja kwa makosa tofauti ikiwemo ya unyang’anyi wa kutumia silaha, kusafirisha dawa za kulevya, ubakaji na ulawiti.
Mbali na hao watu wengine 25 wamehukumiwa Vifungo vya maisha jela kwa makosa ya ubakaji, ulawiti na mauaji.
Akitoa taarifa hiyo leo julai 21, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Justine Masejo amesema kuwa watu hao ni miongoni mwa watuhumiwa 106 waliofikishwa mahakamani kuanzia january hadi juni 2023 kwa makosa ya kihalifu na kupatikana na hatia.
Alisema kuwa mbali na hao, watu wengine 05 wamehukumiwa vifungo vya miaka 20 jela kwa makosa ya kupatikana nyara za Serikali.
"Pia kupitia misako mbalimbali tuliyoifanya katika kipindi hicho dhidi ya madawa ya kulevya tulifanikiwa kukamata Mirungi kilogramu 747 na gramu 695, pia bhangi tani mbili na nusu pamoja na kuteketeza jumla ya tani tano na hekari 60 za bhangi sambamba na Heroine gramu 560.75".
Masejo alisema katika kipindi hicho pia walifanikiwa kukamata watuhumiwa 233 wakiwa na pombe ya moshi maarufu kwa jina la gongo lita 1,091 pamoja na mitambo 21 ya kutengeneza pombe hiyo.
"Mafanikio haya yamekuja
kutokana na ushirikiano wa wananchi kufichua matukio ya haya katika jamii zao
hivyo tunaomba waendelee kusaidia hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi
yao itakayosaidia kupunguza uhalifu mtaani"