![]() | |
Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa |
Arusha
Mkuu
wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amekitaka chuo cha Maendeleo
ya Afya, (CEDHA) kilichopo jijini hapa, kufanya tafiti zaidi zitakazotatua changamoto za sekta ya afya nchini.
alisema majibu ya changamoto katika sekta ya afya yatasaidia
kuepusha wananchi kukimbilia huduma kwa waganga wa kienyeji na watabibu
wasio na taaluma.
Kauli
hiyo ameitoa katika mahafali ya 36 ya chuo hicho ilifanikisha jumla ya vijana 30 wa
ngazi ya stashahada kuhitimu mafunzo ya sayansi ya taarifa ya
afya, walimu wa vyuo vya afya na usimamizi wa afya yanayotolewa kwa kozi
ndefu na fupi.
Alisema
nchi nyingi za Afrika hazina watafiti wa kutosha kutatua changamoto
zake badala yake zinategemea watafiti kutoka nchi zingine kuwaletea
majibu ya changamoto zao jambo ambalo halina tija kwa maendeleo ya taifa
lolote .
"Niombe
sana vyuo hivi ambavyo vinashughulika na magonjwa ya binadamu,
kuzipatia ufumbuzi changamoto za afya zinazotuzunguka na tusipofanya
hivyo tutajikuta tunatupwa nje na sekta yetu itakosa thamani, wananchi
watakimbilia kwa waganga wa kienyeji ambao sio wanataaluma"
Aidha
aliwataka wahitimu wa Mafunzo hayo kuhakikisha wanabeba dhana nzima ya
taaluma ya afya kwa kuyaishi waliofundishwa ili kuvisaidia vituo vya
afya na hospitali hapa nchini kutoa huduma bora na yenye tija.
"Matarajio
yetu, haya mliofundishwa mkayaishi kwa kutoa huduma nzuri ili
mkabadilishe mtazamo kwa baadhi yenu ambao wanaelekea kuichafua taaluma
yenu"
Katika
hatua nyingine alisema kipindi cha mwaka wa fedha, serikali imefanya
maboresho makubwa katika vituo vya afya na zahanati za jiji la Arusha,
ikiwemo kuteta vifaa tiba baada ya kutoa kiasi cha zaidi ya sh, bilioni 6
.
Awali
mkuu wa chuo cha Cedha,dkt Johannes Lukumay alisema kuwa taasisi hiyo
ya Cedha iliyopo chini ya serikali imepewa majukumu makuu manne katika
uanzishaji wake ambayo ni kutoa elimu kwa wakufunzi wa vyuo vya taaluma
ya afya na kuwaendeleza kitaaluma watumishi wa sekta ya afya waliopo
kazini.
Alisema
majukumu mengine ni kufanya tafiti zenye kutatua changamoto katika
sekta ya afya na kutoa ushauri elekezi kuhusu masuala mbalimbali ya afya
hatua ambayo chuo hicho kimefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Alisema
tangu kuundwa kwa taasisi hiyo mwaka 1983 imekuwa taasisi ya kipekee
na yamfano inayotoa mafunzo ya stashahada ya ualimu wa vyuo vya taaluma
za afya nchini Tanzania na visiwani.
Alisema
hadi sasa jumla ya wakufunzi wapatao 617 walihitimu mafunzo katika
taasisi hiyo wakiwemo kutoka nje za nje kama Uganda ,Kenya ,Ethiopia,
Sudan ya Kusini ,Malawi,Namibia na Botswana.
Dkt
Lukumay alisema Cedha imepiga hatua kwa kufanya tafiti wa kuwaongezea
ufahamu wananchi juu ya masuala ya Ukimwi na afya ya Uzazi na
kimeongeza kozi katika nyanja ya tiba ,Kinga na tafiti za afya.
Awali
kwa upande wa wahitimu kupitia risala yao iliyosomwa na mhitimu Joseph
Komba waliiomba serikali kuangalia namna ya kuingiza kozi ya sayansi ya
taarifa ya afya kwenye mfumo wa ajira za serikali ili waweze kupata
ajira pindi wanapohitimu.
"Tangu
kuanzishwa kwa kada ya sayansi ya taarifa ya afya katika chuo cha
Cedha, sisi ni wahitimu wa awamu ya nne na kada hii bado haijaingizwa
kwenye mfumo wa ajira za serikali ,ombi letu tunaomba kada hii iingizwe
kwenye mfumo wa ajira za serikali"