Wanne kuwakilisha nchi Japan

 


BERTHA MOLLEL ,  ARUSHA

Wanariadha wanne nyota wa kimataifa Kutoka Tanzania wanatarajia kukata anga hadi Japan, kushiriki Mashindano ya riadha yanayotarajia kufanyika Octoba 16 mwaka huu.

Wanariadha hao Ezekiel Ng'imba Fabian Joseph, Alfonce Simbu na mwanadada pekee Anjelina John wamepata ualiko wa kushiriki Mashindano ya Jica yanayotarajia kushirikisha nchi mbali mbali.

Msafara huo utakaoongozwa na kocha mwandamizi wa riadha nchini John Francis na balozi wa Jica nchini Tanzania Juma Ikangaa utaondoka nchini Octoba 11 mwaka huu.

Akizungumzia ushiriki wake, Anjelina John alisema kuwa wamejiandaa vema kuhakikisha wanawakilisha nchi vema katika Mashindano hayo ambayo wanakwenda maalum Kwa ajili ya kukuza ushirikiano wa kimataifa.

"Maandalizi Kila siku tunayafanya hivyo sina mashaka na ushiriki wangu katika mbio hizo ambazo tumealikwa"

Simbu alisema kuwa anakwenda kushiriki Mashindano hayo Kwa ajili ya kuendeleza na kukuza ushirikiano baina nchi ya Tanzania na Japan, lakini yeye binafsi atayatumia Kwa ajili Kujinoa zaidi kuelekea Mashindano ya kimataifa.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!