Na Bertha Mollel
Baada ya miaka mitano ya Udhamini wa Sportpesa, Klabu ya Yanga inatarajiwa kusaini mkataba mwingine wa miaka mitano kuendelea na udhamini wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala SportPesa Abbas Tarimba, amesema Mkataba ambao watasaini na Yanga utaweka rekodi kwani hakuna Klabu yoyote hapa Tanzania iliyowahi kupata Mkataba wa aina hiyo.
“Ni kweli mkataba tuliosaini awali umemalizika, Hivi karibuni tutaingia mkataba mwingine mkubwa zaidi na wa kihistoria na klabu ya Yanga SC, ambao haujawahi kuingiwa na klabu yoyote,” alisema Tarimba
Katika mkataba uliopita, Yanga na Simba zilikuwa zikipokea takribani Tsh Bilioni 1 kila mwaka kutoka SportPesa.