Serikali watoa mwongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

 


Arusha. 

Serikali kupitia msimamizi wa uchaguzi, imetoa mwongozo wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024 unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Maelekezo hayo yanayofafanua hatua zitakazoongoza mchakato wa uchaguzi kuanzia uandikishaji wa wapiga kura, uchukuaji na urejeshaji wa fomu za wagombea, uteuzi wawagombea na tarehe ya siku ya uchaguzi una lengo la kutoa mwongozo mzuri utakaohakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, haki na usawa kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa.

Akizungumzia maelekezo hayo,  Leo Septemba 26,2024, ikiwa ni siku 62 kabla ya siku ya uchaguzi, msimamizi wa uchaguzi katika halmashauri ya Meru iliyoko wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, Zainabu Makwinya amesema lengo ni kuhakikisha taratibu zote za uchaguzi zinafuatwa lakini pia wagombea na wapiga kura wanapata taarifa zote zinazohitajika kwa wakati.



Amesema, Wanaoruhusiwa kugombea nafasi za wenyeviti na wajumbe, Makwinya amesema ni Watanzania wenye akili timamu waliofikisha umri kuanzia miaka 21 na kuendelea huku wanaoruhusiwa kupiga kura ni wananchi wenye umri wa miaka 18 na kuendelea na ambao wameshiriki na watakaoshiriki zoezi la uandikishaji wa wapiga kura.

"Fomu za kugombea zitatolewa na kutakiwa kurudishwa kuanzia Novemba Mosi hadi saba mwaka huu kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi ambapo uteuzi utafanyika Novemba nane na siku hiyo tutaanza kupokea mapingamizi kuhusu uteuzi kwa siku mbili hadi Novemba 10" amesema Makwinya.



Amesema kuwa baada ya hapo wataanza kupokea rufaa na kutolewa maamuzi yake kuanzia Novemba 10 hadi 13.

"Baada ya mchakato huo wa uteuzi, kampeni rasmi za uchaguzi zitaanza Novemba 20 hadi 26 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 12"

Amewataka wananchi wote wenye sifa kuhakikisha wanashiriki kwenye mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia hatua za uandikishaji kwenye orodha ya wapiga kura hadi upigaji wa kura.

"Nafasi zinazogombewa ni Mwenyeviti wa Mtaa, wajumbe watano ambao kati yao wajumbe wawili ni wanawake hivyo watu wote washiriki Ili kukuza demokrasia na kuhakikisha upatikanaji wa viongozi Bora kwa maendeleo ya Taifa" amesema Makwinya.

Mwisho...
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!