Gambo atia nia tena Arusha mjini

 

Arusha.

M'bunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo amejitokeza leo kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea kiti chake cha Ubunge awamu ya pili.

Gambo rasmi atachuana na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda na wanachama wengine wa CCM waliochukua fomu tangu June 28,2025 katika Ofisi za CCM Wilaya ya Arusha mjini.


Gambo alishinda kiti hicho cha Ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2000, akimshinda aliyekuwa mgombea wa Chadema Godbless Lema.

katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Timoth Sanga amesema kuwa wako wanachama wengi walioonesha nia ya kutaka kugombea ubunge wa Arusha mjini hivyo atatoa tathimini baada ya zoezi kukamilika.

"Kwa sasa Bado simu ni nyingi hivyo hatuwezi kusema majina hadharani wakati wengine wanakuja, subirini siku mwisho tutatoa majina yote.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post