Na Bertha Mollel
Arusha. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameamua kuvuta fomu ya kuomba ridhaa ya wajumbe wa CCM kumpitisha kuwa mgombea pekee wa ubunge katika Jimbo la Arumeru magharibi.
Sabaya amechukua fomu hiyo Leo June 1, 2025 na kukabidhiwa na Katibu wa wilaya, Camila Kigosi ikiwa imebaki siku Moja pekee kabla dirisha la uchukuaji fomu haujafungwa kwa chama hicho.
Sabaya aliyekuwa ameongozana na mkewe,Jesca Thomas, aligoma kufanya mahojiano na waandishi wa habari huku akisimamia msimamo wake kuwa anamuachia Mungu.
"Sina cha kuzungumza, Ninamuachia Mungu afanye kazi yake,mbarikiwe sana"alisema Sabaya na kuondoka.
Sabaya ni miongoni mwa watia nia 20 waliojitokeza kuwania jimbo hilo wakiwemo wafanyabiashara na wasomi mbalimbali