Na Bertha Mollel
Arusha. Hatimae Dk Ojung'u ole saitabau amerusha fomu Leo June 1,2025 aliyochukua ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa na wajumbe kuipeperusha bendera ya CCM katika kinyang'anyiro cha Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi.
Dk Ojung'u Ole Saitabau ni miongoni mwa makada 20 wa CCM waliojitosa Kugombea Uteuzi wa Ubunge jimbo la Arumeru Magharibi iliyoko Mkoa wa Arusha.
Ojung'u ambaye pia ni mwanasayansi mbobezi wa masuala ya Jografia na maendeleo, ameahidi kuleta mageuzi ya kweli ya kiuchumi na maendeleo jumuishi kwa wananchi wa jimbo hilo.
Amesema amefikia hatua hiyo ikiwa ni kuitikia Sauti ya wito wa kuwatumikia wananchi wa Arumeru magharibi katika changamoto mbalimbali wanazopitia.