Bertha Mollel
Mkurugenzi wa Utawala SportPesa Abbas Tarimba amethibitisha kumalizana na Klabu ya Simba katika mkataba wa Sport Pesa.
Aidha mkataba huo uliodumu kwa miaka mitano, Simba SC ilikuwa inavuna kiasi cha shilingi Bilioni moja kila mwaka kutoka kwa SportPesa
kutokana na kumalizika kwa mkataba huo, Tarimba amethibitisha kutokuongezana hivyo Kuitakia kila la kheri Simba SC kwa maisha ya nje ya mkwanja huo.
Tarimba alisema pande zote zimeridhika kwa huduma iliyotolewa kwa kipindi chote na wanaamini Simba SC itaendelea kuwa mfano wa kuigwa katika udhamini uliokuwepo kati yao.
Aliongeza kuwa wanajivunia mafanikio makubwa waliyoyapata wakiwa na Klabu ya Simba SC, na hata upande wa Klabu hiyo ana uhakika utakuwa umefurahia kufanya kazi na kampuni hiyo ya Michezo ya kubashiri nchini.
“Ni kweli tumemaliza Mkataba wa Simba SC, tumekuwa nao kwa kipindi Kirefu, sisi tulikua na matarajio ambayo tulipenda yafanyike na wao ilikua hivyo pia,”
“Naweza kusema kwamba tuheshimu maamuzi yaliyofikiwa na pande zote mbili, tunaitakia kila la kheri Simba SC katika mpango wake ndani na nje ya uwanja.” amesema Tarimba