Dc Meru ataka bweni lituzwe lisaidie wanafunzi wengi



picha mbali mbali katika uzinduzi wa Bweni 



Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango amewataka watumishi katika  shule ya Sekondari Nkoasenga kutunza miundo mbinu ya bweni walilokabidhiwa ili kusaidia wanafunzi wengi waliopo sasa  na watakaokuja.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa  Hosteli ya wasichana, yenye jumla ya  vyumba 12 (self contained ) vitakavyotumiwa na  wanafunzi 48 katika shule ya Sekondari Nkoasenga.

Mhe.Mhandisi Ruyangu amesema kuna maboresho makubwa katika sekta mbalimbali yaliyofanywa na  Serikali ya awamu ya sita,ambapo katika shule ya Nkosenga imenufaika na chumba kimoja cha darasa  katika bilioni 1.4 ya ujenzi wa madarasa 70 zilizotolewa na Serikali  katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

Aidha,Ruyango ameutaka uongozi wa shule kutunza miundombinu ya Hostel hiyo ambayo   imejengwa  na  wadau marafiki wa Kijiji cha Nkoasenga kutoka Ujerumani (ASANTE SANA) kwa kushirikiana wanajamii wa Nkoasenga ambapo marafiki hao wamechangia zaidi ya Shilingi Milioni mia 259.9.

Aidha, awali kiasi cha Shilingi Milioni 20 kiliitajika kwa ajili ya ununuzi wa eneo la kujenga hosteli ambapo Mhe.John D. Pallangyo mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki alichangia  Shilingi Milioni 10, Halmashauri Shilingi milioni 1 na kiasi kilichobaki kilichangwa na jamii kupitia harambee na michango mbalimbali.

Hosteli hiyo ni chachu katika kuendelea kuinua taalum kwani itaondoa changamoto ya wanafunzi wa kike kutembea  umbali mrefu kwenda shule na kurudi majumbani nk.

Hosteli  hii mbali na kuwa na vyumba 12 vyenye vya wanafunzi 48 ina  chumba cha Matron, chumba cha wagonjwa wenye maradhi ya kuambukiza (Isolation room) ,chumba cha kufulia (laundry) ina nishati ya umeme ,lina mfumo wa solar utakaotumika kuchemsha maji ya kuoga nk.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe.Mbunge Dr.John  Pallangyo,Mh.Diwani Kata ya Leguruki,Wadau kutoka Ujerumani, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Meru,Viongozi wa Chama Kata  Leguruki na Kijiji cha Nkoasenga Pia viongozi wa dini ,wananchi, Wazazi na Walezi wa Wanafunzi.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!