CCM wamuombea kibarua kipya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa

 



Arusha. 

Chama cha mapinduzi kimempigia magoti Rais Samia Suluhu Hassan kumpatia kibarua kingine aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa.

CCM wametoa Ombi hilo leo January 29,2025 kwenye makabidhiano ya Ofisi kati Mtahengerwa na Mkuu mpya wa Wilaya Joseph Mkude aliyeteuliwa akitokea Wilaya ya Kishapu.

Mtahengerwa aliyehudumu katika Ofisi ya Ukuu wa Wilaya ya Arusha kwa miaka miwili pekee tangu January 25,2023 alipoteuliwa, ameondoka rasmi katika nafasi yake January 24,2025 baada ya kutenguliwa na Rais Samia.

Akizungumza katika makabidhiano ya Ofisi hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha, Willfred Soilel Mollel amesema kuwa uamuzi wa Rais Samia kumtengua mkuu huyo ingawa hawawezi kubishana nao lakini wanachoweza ni kumuomba ampe kibarua kingine.

"Utenguzi huu sisi hatuna la kusema, kwa sababu aliyekelekeza ni Rais wetu ambae hatuwezi kum'bishia kwa hili, ila tunachoweza ni kumuomba ampe Felician (Mtahengerwa )kibarua kingine kwani Bado ni kijana na ana nguvu anaeweza kufanya kazi Bado" amesema Soilel.

Nae Mtahengerwa amesema kuwa anawashukuru watumishi wenzake kwa ushirikiano alioupata kwa mda wote aliofanya kazi katika nafasi yake ya Ukuu wa Wilaya.

Nae Mkude akipokea kijiti hiko ameshukuru kwa mapokezi mazuri ya watumishi wenzake na kuomba ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.

"Mimi ndio kwanza mgeni, Sina ninachojua hivyo ninapomkimbilia yoyote kati yenu kuomba msaada wa jambo naombeni ushirikiano kuhakikisha wilaya yetu inafanikisha malengo yake ya hasa miradi ya maendeleo na utatuzi wa kero za wananchi" amesema.

Mwisho

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!