NCAA wafichua fursa za uwekezaji ndani ya eneo la Ngorongoro

 


Arusha 

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro  (NCAA) imefanikiwa kutangaza fursa za uwekezaji katika mkutano wa Nishati unaohusisha wakuu wa Nchi za Africa (Africa Energy Summit) uliofunguliwa na Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko.

 Mkutano huo unaoendelea katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam umewakutanisha wakuu wa nchi zaidi ya 25 barani Afrika, wawakilishi wa wakuu wa nchi na mashirika ya kimataifa ambapo Tanzania ni Nchi mwenyeji.

NCAA inashiriki mkutano huo kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani na nje ya hifadhi ya Ngorongoro na kuelezea wageni shughuli za utalii zinazofanyika ndani ya hifadhi.

 Miongoni mwa shughuli hizo ni utalii wa picha,  utalii wa utamaduni na mambo kale, utalii wa miamba (Geo tourism), Utalii wa anga (Astro tourism) kupitia Kimondo cha Mbozi, utalii wa kutembea (walking Safaris), utalii wa kupanda milima (hiking), utalii wa puto (Balloon Safaris) pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo Ngorongoro.

Aidha NCAA kupitia mkutano huo inatumia fursa kutoa mualiko kwa wageni mbalimbali wanaoshiriki kutembelea eneo la Ngorongoro hususan eneo la Ndutu ambapo msimu huu ni mahsusi kwa Nyumbu wanaohama ambao wanaendelea kuzailiana kwa wingi katika eneo la Ndutu.

Mwisho..

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!