Yanga kuburuzwa FIFA


YANGA yasitisha safari ya UturukiBaada ya Uongozi wa Klabu ya Yanga SC kufuta safari yao ya kwenda nchini Uturuki Kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao (Pre-season), kampuni ya ENDA TOUR imepanga kuwashitaki mabingwa hao wa ligi kuu na kombe la shirikish la Azam kwa TFF na FIFA.

Kampuni ya ENDA TOUR imepanga kuwashitaki klabu ya Yanga kwa TFF na FIFA ili kudai fidia ya milioni 200 kwa klabu hiyo kwa kukiuka makubaliano ya kimkataba waliyokubaliana hapo awali.

 Yanga ambao wamepanga kwenda mkoani Morogoro kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao, awali walikuwa na mipango ya kwenda nchini Uturuki ambapo inaelezwa kuwa waliweka oda (Booking) ya mahala pa kufikia.

Inadaiwa kuwa klabu ya Yanga waliingia mkataba wa makubaliano na Kampuni hiyo ili waandaliwe kambi ya mazoezi (Hoteli, Viwanja) na mechi za kirafiki wakati wakiwa Uturuki kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao (Pre-season).

Yanga walipanga kuanza kambi hiyo tarehe 15/07/2022 hadi 04/08/2022.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!