KIKOSI cha Simba kiliondoka nchini jana Alhamisi jioni kwenda Mjini Ismailia nchini Misri kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022/2023.
Simba imeondoka na wachezaji wake wote, wakiwemo wapya, wazawa wawili, kiungo Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar na mshambuliaji Habib Kyombo kutoka Singida Big Stars FC iliyomsajili Kutoka Mbeya Kwanza FC iliyoshuka Daraja msimu uliopita wa 2021/2022.

Wengine ni wageni kiungo Mnigeria, Victor Akpan kutoka Coastal Union, winga Mghana, Augustine Okrah kutoka Asante Kotoko ya kwao na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri kutoka Zanaco ya kwao.
Wengine ni Shomary Kapombe, Ally Salim, Benno Kakolanya, Jonas Mkude, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Pape Sakho, Chris Mugalu, Meddie Kagere, Jimson Mwanuke, Chama, John Bocco, Israel Mwenda, Joash Onyango na Henock Inonga.
Kikosi hicho chini ya kocha mpya, Mserbia Zoran Manojilovic ‘Maki’ kinatarajiwa kurejea nchini August 5,2022 kwaajili ya Tamasha lake la Simba Day siku tatu baadaye.
Baada ya kuwasili salama kwenye Mji wa Ismailia, Misri, huu ni utulivu wa eneo hilo ambalo Simba imeweka kambi ya maandalizi yake.
Simba itakuwa hapa kwa takribani wiki tatu kujiandaa na msimu mpya wa 2022/2023.
Kambi ya maandalizi ya msimu mpya iliyopo jijini Ismailia, Misri.
Kikosi cha Simba SC kimeanza rasmi (Pre-Season) katika mji wa Ismailia nchini Misri kujiandaa na msimu mpya wa mashindano 2022/2023