Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere akikata utepe wa kuzindua mpango mkakati wa Tasta.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara akikabidhi mpango mkakati wa Tasta kwa mdau wa mbegu.
Na Mwandishi wetu -Manyara
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amesema Tanzania itafikia lengo la
kuwa na uhakika wa usalama wa chakula kwa kusimamia sera na miongozo ya
uzalishaji wa mbegu bora zitakazotosheleza mahitaji ya ndani na
kuondokana na dhana ya kutegemea kuagiza pembejeo za kilimo kutoka nje
ya nchi.
Makongoro ametoa rai hiyo jijini Arusha wakati wa
ufunguzi wa kongamano la wadau wa mbegu waliokutana kwaajili ya kujadili
ufanisi katika ushirikiano na serikali kwenye kuboresha mazingira ya
kisera na udhibiti kwenye sekta ya mbegu.
Amesema kuwa sera na
miongozo ya nchi katika sekta ya kilimo hususani mbegu inatakiwa
isimamiwe imara ili kuwa na mbegu bora ambayo itatoa mazao bora
yatakayosaidia kukuza uchumi wan chi pamoja na kipato cha mkulima.
‘’Ni
wakati sasa wa wazalishaji wa mbegu kujikita kutengeneza mbegu bora ili
jamii na nchi za jirani ziweze kujua kuwa mbegu bora zipo
Tanzania’’Alisema
Amesema kuwa katika suala la kilimo siasa
inabidi kuondoka ili kuwezesha kilimo kuwa cha kibiashara na kunufaisha
jamii ya watanzania na wakulima wenyewe ambao wanapambana kuhakikisha
wanapata mazao bora yatakayokuwa na tija.
Awali akielezea kuhusu
muelekeo wa Tanzania kwenye sekta ya mbegu afisa mtendaji mkuu mpango wa
kukuza kilimo ukanda wa kusini mwa Tanzania SAGCOT Geofrey Kirenga
amesema kwa kutekeleza dhana ya ushirikishwaji Tanzania imekuwa moja ya
nchi za mfano wa kuigwa.
Aidha amesema kuwa wakulima wasipotunza
udongo kwa uhakika kupata mbegu bora itakuwa historia kutokana na
wakulima kupaswa kupata elimu kutoka kwa maafisa ugani ambapo wakulima
na maofisa ugani kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa na mbegu bora.
Taasisi
yenye jukumu la kusimamia makampuni ya uzalishaji na uagizaji wa mbegu
nchini [TASTA] Bob Shuma ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo
wanasema ushirikiano wa serikali katika sekta hiyo ya mbegu umekuwa wa
mafanikio na matokeo chanya.
Amebainisha kuwa Tasta kwa sasa
imekuwa ya pili barani Afrika kwa kusimamia sekta ya mbegu ikifatiwa na
nyingine iliyoko south Afrika ambapo anasema hiyo yote imetokana na
kufanya kazi na serikali kwa karibu pamoja na wadau wa mbegu na hiyo
ndiyo siri ya mafanikio hayo.
Amesema misingi imara inapaswa
kuboreshwa kwa kushirikiana na serikali ili kuweza kuwezesha vizazi
vijavyo kujivunia uwepo wa TASTA kwa kuweza kutekeleza majukumu yake kwa
kuitaka serikali kuendelea kufanya kazi na sekta binafsi ili kuweza
kufika mbali.
Washiriki wa kongamano la wadau wa mbegu wakifatilia mijadala inayojadiliwa kuhusu mbegu.