Ngono watajwa utumwa mwingine kwa wafanyakazi wa ndani

mkurugenzi wa shirika la AMATA, Bernadette Clementi akitoa mafunzo ya kujitambua na kujithamini kwa wafanyakazi wa ndani


Bertha Mollel, Arusha


 .Wafanyakazi wa ndani wamesema kuwa licha ya kufanya kazi ngumu za majukumu ya nyumbani na malezi lakini pia baadhi yao wamekuwa wakitumikishwa kingono na wanafamilia wa kiume kazini.



Wamesema kuwa utumwa huo unatekelezwa na wanaume wa familia za nyumba wanazofanyia kazi, kwa ushawishi wa ahadi za uongo za kifedha au ndoa lakini wakati mwingine kwa matisho ya kunyang'anywa ajira zao au hatarisha uhai yao.


Wafanyakazi hao wamesema hayo jijini Arusha kwenye mafunzo ya siku moja iliyotolewa na Taasisi ya Ajira na maendeleo Tanzania (AMATA) namna wanavyoweza kujitambua na kujithamini kazini ikiwemo kuepuka vishawishi vinavyoweza kuharibu ujira wao.

Blandina Anthony mmoja wa wafanyakazi 30 waliopatiwa mafunzo hayo, ambapo alisema kuwa kazi za ndani zimeghubikwa na viatarishi vingi hasa vya ukatili wa vipigo na utumwa wa kingono hivyo kuomba mabosi zao wa kike kuwa karibu nao zaidi ili waweze kuwasaidia.

"Hii kazi ni ngumu kutokana baadhi ya wanafamilia tunaowatumikia wanavyotuchukulia kama watumwa hivyo tunaomba  mabosi zetu wamama wawe karibu na sisi wasitupige ili kutusaidia tunapokumbwa na changamoto yoyote ya kutakwa kimapenzi na waume zao au wanafamilia yoyote ikiwemo ndugu na watoto wao wa kiume" 

Alisema kuwa ukaribu na kusaidiwa kuepukana na matukio ya ukatili unawaweka salama hata familia zao lakini utekelezaji wake huweza kuleta madhara makubwa ikiwemo baadhi ya wasaidizi hao kutaka kulipiza kisasi kwao.


Naomi Shedrack kutoka Ngaramtoni aliwataka mabosi zao kutumikia na kushika Imani za kidini kutokana na baadhi ya wasaidizi wanaowaleta wanatumwa kimaslahi ikiwemo kuteka nyumba au familia kwa nguvu za giza.

"Mimi niwaombe tu wawe na Imani za dini na kusali Sana maana Mimi nilishawahi kushuhudia mfanyakazi mwenzangu anaongea na sim na bibi yake aliyemleta kufanya kazi kumbe alikuja kuiba watoto kichawi" alisema na kuongeza ...

"Lakini pia baadhi ya mama zetu wanatuma mabinti zao kwenye kumtongoza baba mwenye nyumba ili amuache mkewe na awe nae huyo binti" alisema.
mkurugenzi wa shirika la AMATA, Bernadette Clementi



Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la AMATA, Bernadette Clementi alisema mafunzo hayo wanalenga kuwasaidia wafanyakazi wa majumbani waweze kujitambua na kuthamini kazi zao kwa kuiona ni ajira kama ajira zingine halali zinazowaingizia kipato.


Alisema baadhi ya wafanyakazi wa majumbani wameshindwa kuithamini kazi hiyo kwa sababu za kimtazamo wakiamini kazi za ndani wanafanyia shida nani utumwa hivyo kushindwa kuyafikia malengo yao ya kimaisha kupitia ujira huo .

"Lakini pia hapa tunawafundisha umuhimu wa kuwa na mahusiano mazuri baina yao na waajiri wao ili kuondoa hali ya sintofahamu na tukimaliza hapa tutawageukia waajiri wao kutambua umuhimu wa mabinti zao wa kazi" alisema 

 
Mwisho....

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!