kampuni ya mabasi ya coast liner watoa msaada wa jezi kwa timu ya soka walemavu Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela akipokea vifaa kutoka kwa meneja wa kampuni ya mabasi ya coast liner, Zohra Ally kabla ya kukabidhi kwa walengwa


 Mkoa wa Arusha imeunda rasmi timu ya soka ya Walemavu na inatarajia kuwakilisha mkoa kwa Mara ya kwanza kwenye mashindano ya ligi ya Taifa inayotarajiwa kufanyika jijini Dar-es-salaam mapema mwezi agost mwaka huu huku  kampuni ya mabasi ya cost liner, ikiwavalisha jezi mapema.


Timu hiyo mpya iliyoundwa hivi karibuni na kuitwa 'Arusha Warriors Amputee Sports Club', imeundwa na jumla ya watu wenye ulemavu 19 na imeanza kujinoa vema katika viwanja vya Sheikh amri Abeid.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa vifaa vya michezo na kampuni ya mabasi ya cost liner, katibu wake Abdulaziz Ally alisema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuhakikisha mkoa haukosi uwakilishi katika mashindano mbali ya kitaifa na fursa za kimataifa.

"Timu imeanza mazoezi hapa Sheikh amri Abeid katika maandalizi ya matukio kadhaa ya kimichezo ikiwemo Ligi ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu Tanzania Bara, Kombe la Taifa lijalo pamoja na Ndondo Football Cup 2023 lengo ni kuhakikisha Arusha hatupotezi fursa yoyote ya michezo".

Akikabidhi vifaa hivyo kwa mkuu wa mkoa, meneja wa kampuni ya mabasi ya coast liner, Zohra Ally alisema wameguswa kutoa vifaa hivyo ikiwa ni utamaduni waliojiwekea ya kurudisha faida kwa jamii.

"Leo tumetoa seti ya jezi, viatu vya soka na soksi kwa timu hii ya Walemavu ikiwa ni desturi yetu ya kurudisha faida kwa jamii hivyo tunawaomba timu hii wahakikishe wanafanya vema kwenye mashindano yao ili kuvuta na wadau wengine kuwa karibu nao"

Akipokea vifaa hivyo na kukabidhi kwa walengwa ( Arusha Warriors Amputee Sports Club), mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela aliishukuru kampuni ya coast liner kwa kusaidia timu hiyo na kuwaita Wadau wengine kusapoti juhudi za mkoa katika kukuza michezo.

"Hakuna jambo zuri kama kuona juhudi za serikali na kusaidia itimie haraka hivyo kampuni hii imefanya jambo zuri niombe wadau wengine wajitokeze kuhakikisha timu hii inapata nafasi ya kuwakilisha mkoa vema kwenye mashindano mbali mbali ya kitaifa na kimataifa hapo baadae"

Nahodha wa timu hiyo, Ibrahim Mloe amesema kuwa kuanzishwa kwa timu hiyo miezi miwili iliyopita imekuwa fursa kwa vijana wenye ulemavu ambao vipaji vyao vya soka vilikuwa vikipotea kwa kukosekana jukwaa la kuonyesha.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!