Wanafunzi wa Korea wachangia milioni 100 kujenga madarasa Tanzania

sehemu ya wanafunzi kutoka Korea waliokuja nchini kutoa msaada wa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa matano wakiwa wanachimba msingi wa ujenzi huo


Wanafunzi hao wa Korea waliochangia wenzao milioni 100 wakishiri kuchimba msingi wa madarasa 

Mwalimu mkuu wa shule ya Saeronam ya nchini Korea,  Sung Hee (kulia) akishuhudia ujenzi huo

Bertha Mollel, Moshi.


 Jumla ya watoto 27 Kutoka nchini Korea waliohitimu Elimu yao ya juu katika shule ya Saeronam international school wamefanikiwa kuchangishana zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kusomea watoto na vijana wenye mahitaji hapa nchini.

Mbali na kuchangia kiasi hicho cha fedha, vijana hao pia wamekuja hadi hapa nchini Tanzania kwa ajili ya kuchangia pia nguvu kazi ya ujenzi wa madarasa hayo lakini pia kutembelea vituo vinavyowalea.

Wanafunzi hao Kutoka Korea wenye umri Kuanzia miaka 15 hadi 17, wametoa fedha hizo katika zoezi la uchangishaji wa fedha Kwa ajili ya kuwasaidia watoto na vijana wa kitanzania wenye mahitaji lililoratibiwa na Shirika la compassion international Tanzania Kwa kushirikiana na compassion Korea na shule ya Saeronam international high schoo.


Akizungumza baada ya kutua nchini Tanzania Kwa ajili ya kutoa mchango huo, mwalim mkuu wa shule ya kikristo ya 'Saeronam ', ya nchini Korea, Sung Hee alisema kuwa wanafunzi wao wametoa mchango huo kama sehemu ya kurudisha shukrani Kwa Mungu kwa kuwasaidia kuhitimu Elimu salama.


"Kutoa shukrani Kwa Mungu kupitia kuwasaidia watu wahitaji ni Moja ya mambo tunayowafundisha wanafunzi wetu, hivyo katika kuhitimu Elimu yao wakaona tuje Tanzania tutoe msaada huu wa kuwasaidia wenzetu wa shirika la kikristo wenye kuhitaji msaada wa kuwasaidia watoto na vijana wenye maisha magumu"


Kwa Upande wake Merry Mwabukusi Kutoka shirika la compassion Tanzania alisema kuwa mchango walioutoa wanafunzi hao Kutoka Korea unaelekezwa kwenye ujenzi wa madarasa matano na ofisi Moja ya walimu katika  kituo cha huduma ya watoto na vijana katika kanisa la TAG lililoko Mailisita mjini Moshi.


"Madarasa hayo ni ya kuwahudumia watoto na vijana wahitaji ambao wamekuwa wakifundishwa Elimu mbali mbali za kibiashara, ujasiriamali na Elimu ya kiroho katika huduma za kijamii"


Alisema kuwa ujenzi huo ni Moja ya miradi yao ya kuishika mkono serikali katika maeneo ambayo hayajafikia kielim, huduma za kijamii, kukuza vipaji na maadili katika jamii hasa za kimaskini.

Alisema kuwa wanahudumia mikoa 21 ya Tanzania ndani ya makanisa 520, na watoto 112,000 katika nyanja mbali mbali.


Kwa Upande wake mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG, Maili sita Elishadai, Semu Bukuku alisema kuwa waliazisha kituo cha kusaidia watoto wenye mahitaji mtaani na walikuwa na upungufu wa madarasa ambapo awali walikuwa wanatumia madarasa ya shule ya msingi njoro.


Alisema  walinunua kiwanja kwa mchango wa waumini wa kanisa na wakaomba msaada wa kujengewa madarasa ambapo ni  hilo liliwagusa shirika la compassion Tanzania na kuwamua kuwasaidia.


"Madarasa haya yatatumika kuwafundisha watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwapeleka shule ambapo watahakikisha wanafikia malengo yao ya kimaisha Kwa Elimu mbali mbali wanayotoa katika kituo ikiwemo maadili, afya, ujasiriamali, biashara Ili waweze kuwa na sifa za kuajiriwa wanapohitim Elimu zao lakini pia kujianjiri katika fani ya malengo ya maisha yao"


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!