![]() |
BERTHA MOLLEL, ARUSHA
Akizungumzia safari hiyo, mwenyekiti wa chama Cha baiskeli mkoa wa Arusha, Mosses Andrea alisema kuwa wameondoka mapema Ili Octoba 14 iwakute eneo la tukio (Butiama Kijiji Cha Mwitogo ilipo kaburi lake) ambapo ndio maadhimisho rasmi ya kumbukumbu ya hayati Mwalimu Nyerere.
"Tunaondoka Leo (Jana) tutalala Babati, kabla ya kuelekea kondoa na kukutana na wenzetu wa Dar-es-saalam mkoani Dodoma ambapo tutaungana nao kuelekea Mwanza tutakapoungana na wenzetu na kuondoka pamoja hadi Mara"
Alisema kuwa lengo la kuendesha baiskeli hadi lilipo kaburi la baba wa Taifa, ni kumuenzi Kwa vitendo kuendeleza mchezo wa baiskeli aliokuwa anaupenda Mwalimu Nyerere, kutokomeza ujinga Kwa kuchangia madawati katika shule mbali mbali nchini kunakofanyikia kampeni hiyo, lakini pia kuhamasisha utalii na afya.
"Ikumbukwe kuwa Mwalimu alikuwa anaupenda kuendesha baiskeli Kila alipokuwa akienda, ndio tukaona sisi waendesha baiskeli tuna jukumu hili, lakini pia tunaenzi mambo yake ya kufuta ujinga Kwa kuwapa fursa wanafunzi kupata madawati ya kukalia na zaidi tunahamasisha utalii na kuboresha afya zetu pia kupitia safari hii"
Alisema kuwa watakuwa pia na zoezi la kuotesha miti katika shule watakazogawa madawati kabla ya kuhitimisha katika shule iliyoko katibu na Kijiji Cha Mwitogo alikozikwa hayati baba wa Taifa.
Mmoja wa wachezaji hao, Bashiru Shah alisema kuwa wanajisikia vizuri kumuenzi baba wa Taifa Kwa vitendo ambapo wanatarajia kufanya makubwa msimu ujao zaidi.
'hayati Mwalimu Nyerere ni Rais wetu wa kwanza Tanzania hivyo kumuenzi Kwa kuratibiwa jambo kama hili tumefurahi sana kikubwa tunaomba wananchi wengine watusapoti Kwa kuchangia madawati Ili kutimiza kampeni yetu ya "changia madawati kutokomeza ujinga' "