![]() |
Mkurugenzi Msaidizi wa usalama mtandao kutoka Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi Stephen Wangwe,akizungumza leo jijini Arusha. |
Bertha Mollel , Arusha.
Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari wamawatahadharisha wana vyuo kuwa makini na matumizi
ya mitandao ikiwemo kujiridhisha na madhumuni ya kila wanachotaka kuchapisha ili kujikinga na uhalifu sambamb na dhima za udhalilishaji, utapeli na
udukuzi wa taarifa binafsi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtanda kutoka , Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari , Mhandisi Stephen Wangwe, kwenye semina ya kuwajengea uelewa wanafunzi na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC),kuhusu usalama mtandao.
Alisema kuwa Udhalilishaji
mtandaoni,utapeli na udukuzi wa taarifa binafsi zimekuwa miongoni mwa changamoto
za kimtandao hapa nchini hivyo ni vema watumiaji wa mtandao kuwa makini kabla
ya kuchapisha jambo lolote ili kujikinga na matukio hayo.
"Kimsingi hili ni janga la
dunia na hapa nchini maeneo matatu yamekithiri sana la kwanza ni udhalilishaji
mtandaoni hili tumeliona likikua kwa kasi sana,kunyang'anywa akaunti ambapo
wamekuwa wakiombwa taarifa zao kumbe sio kwa watoa huduma na la tatu ni utapeli
kuna zile meseji maarufu ile hela tuma kwenye namba hii,siku hizi wengine
wanajifanya waganga,"amesema
Amesema lengo la mafunzo hayo ni
kupunguza matukio ya uhalifu mtandaoni kwa kujenga uelewa kuhusu mbinu
zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni, namna wanavyoweza kubaini mashambulizi
ya mtandao na masuala gani wanayoweza kufanya ili kujikinga dhidi ya uhalifu wa
mtandao.
Amesema serikali ina mkakati wa
taifa wa elimu kwa umma wa usalama mtandao ambapo wanatarajia kufikia makundi mbalimbali
ikiwemo vijana,wazee na makundi ya wenye mahitaji maalum wakiwemo watu wenye
ulemavu na kuwa watawaandalia maudhui maalum ili elimu ya kujikinga mtandaoni
iwafikie wote.
Kwa upande wake Mkuu wa ATC, Musa
Chacha, alisema kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo,kupitia idara yao ya Tehama
wataongeza suala la usalama mtandao na kufundisha wanafunzi wao kwenye masomo
ya kawaida.
"Mafunzo haya ni muhimu
sana na sisi kama wadau na watumiaji wazuri wa mtandao,hata
shughuli za chuo zinaendeshwa kwa njia ya mtandao,hivyo ni muhimu kwetu
ili tuweze kujilinda na uhalifu wa mtandao,"amesema
Naye mtaalam wa usalama mtandao ya
uchunguzi wa makosa ya kidigitali,kutoka Wizara hiyo,Yusuph Kileo,amewataka
wananchi kutambua kilo mmoja ana jukumu la kujilinda kwenye mtandao,kuhakikisha
wanatumia nywila madhubuti ili wabaki salama kwenye mtandao.
Amesema moja ya changamoto kubwa ni
pamoja na watu wengi kutokuripoti matukio hayo na kuwa chanzo cha wahalifu
kuendelea kudhuru wengine.
"Tumekuwa tukihamasisha watu
wawe makini wanapofanya mambo yao mtandaoni mfano kuangalia taarifa gani
wanaweka mtandaoni isije kuwa chanzo cha wao kuwa wahanga wa mtandaoni,
tunahamasisha watu wawe na tabia ya kuripoti haya matukio ya uhalifu
mtandaoni,"