Rais Samia awaitia wawekeza fursa za utalii

  


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani, Zurab Pololikashvili  baada  ya kufungua Mkutano wa 65 wa Shirika  la Utalii Duniani – Kamisheni ya Afrika kwa niaba ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan   uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia jijini Arusha, Oktoba 5, 2022. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi  Dkt. Pindi Chana.

Bertha Mollel, Arusha


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wadau wa utalii duniani kuja nchini kutumia fursa za uwekezaji zilizoko Tanzania Kwa maendeleo ya pande zote mbili.

 
Rais Samia aliyewakilishwa na Waziri mkuu Kasimu Majaliwa kwenye mkutano huo, amesema kuwa sababu kubwa mbali na fursa na rasilimali za uwekezaji lakini pia Tanzania ni nchi yenye amani na utulivu tena yenye watu wenye ukarimu .

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo Leo Octoba 5 wakati akifungua mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) Kamisheni ya Afrika, wenye kauli mbiu ya "Kujenga upya  ustahimilivu  wa utalii  wa Afrika Afrika ajili ya maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi," .

Katika mkutano huo wa siku tatu inayoendelea mkoani Arusha,  Majaliwa alisema Tanzania ina maeneo mengi yaliyo wazi yanayofaa Kwa  uwekezaji wa sekta mbali mbali hasa utalii hivyo kuwaomba wajumbe hao kutumia fursa hiyo Kwa manufaa ya Tanzania na muwekezaji.

"Najua mtapata nafasi ya kutembelea baadhi ya maeneo ya vivutio vyetu, Sasa naomba msiishie kujifunza bali mtumie kama fursa"

Mbali na hilo Majaliwa alisema takwimu za mwaka 2021 zinaonesha kuwa watalii wanaokuja nchini Tanzania wameongezeka kwa asilimia 48.6 kutoka watalii 620,867 mwaka 2020 na kufikia watalii 922,692 mwaka 2021.

Mheshimiwa Majaliwa amesema mbali na kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini, pia mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kwa asilimia 81.8 kutoka Dola za Marekani milioni 714.59 mwaka 2020 na kufikia Dola za Marekani bilioni 1.3 mwaka 2021.

“Pia takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa Sekta ya Utalii inazidi kuimarika zaidi hususan baada ya uzinduzi wa Programu Maalumu iliyotekelezwa na Mheshimiwa Rais Samia ya The Roya Tour iliyozinduliwa rasmi Aprili 2022 katika soko letu la utalii la kimkakati nchini Marekani


Aidha amepongeza uamuzi wa Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) na washiriki wake kuunga jitihada za Tanzania kutunza mazingira kwa  kupanda miti baada ya mkutano huo.



 Kwa Upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana alisema mkutano huo umehudhuriwa na waziri  33 kutoka nchi wanachama  wa UNWTO  ukanda wa Afrika mwenye dhamana ya utalii pamoja na wageni wataalamu wa masuala ya  Maliasili.

Alisema katika mkutano huo ni kujadili kuhusu mustakabali wa ustawi wa maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika hasa baada ya athari za mlipuko wa janga la uviko -19 ilivyokuwa imeathiri utalii wa kimataifa Kwa wastani wa asilimia 50 Hadi 85 katika nchi mbali mbali.

"Katika mkutano huo tutakuwa na matukio mbali mbali ikiwemo hafla ya ufunguzi, kutakiwa na zoezi la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini kupitia jukwaa la uwekezaji, lakini pia wadau wa utalii watajengewa uwezo kuhusu maswala ya masoko na zaidi kutakuwa na ziara ya mafunzo ambapo tutatumia kutangaza vivutio vilivyopo nchini"

Waziri Chana alisema kuwa Tanzania wanatarajia kutumia mkutano huo mkubwa duniani kama fursa ya kutekeleza sera ya Taifa ya kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia milioni 5 na mapato ya Dola billioni 6 ifikapo mwaka 2025.

" Mkutano huu kama nchi tutautumia Kwa manufaa makubwa kiutalii na kiuchumi katika kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan aliyeanzisha kupitia filamu yake ya 'the Royal tour' ambapo Kwa sasa tunaendelea kutanua wigo wa mazao ya utalii nchini"

Kwa Upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha aliwataka wananchi wa mkoa huu kuonyesha ukarimu Kwa wageni hao huku akiahidi kulinda ulinzi na usalama wao wote Kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

"Kikubwa wakazi wa Arusha wachangamkie fursa zitokanazo na mkutano huu Kwa watu wa hotel, migahawa, wasafirishaji na wengine pia tuendelee kulinda taswira ya mkoa na nchi Kwa ujumla Kwa kuwa wakarimu Kwa wageni bila bugha yoyote


Kwa Upande wake mwenyekiti wa kamisheni ya utalii Zanzibar Rahim Bhaloo alisema kuwa mkutano huu umekuwa fursa kubwa kwao kujifunza mengi Kutoka Kwa wataalamu wa maswala ya utalii duniani.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!