Rais Samia kuwa mgeni rasmi mkutano wa UNWTO-CAF,

 

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan


BERTHA MOLLEL , ARUSHA

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano  wa Kimataifa wa 65 wa shirika la Utalii duniani kamisheni ya afrika unaotarajia kufanyika  octoba 5 Hadi 7 mwaka huu mkoani Arusha

Mkutano huo wa siku tatu unatarajia kukutanisha mamia ya wadau wa Utalii na maliasili wakiwemo mawaziri wa nchi 50 wa afrika, wawekezaji katika utalii, wataalamu katika mnyororo wa utalii na wageni wengine.

Aidha Tanzania imepewa jukumu la kuwa mwenyeji wa mkutano huo wa UNWTO-CAF) na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia  maswala ya Utalii wakiwa na kauli mbiu  'rebuilding Africa's tourism resilience for inclusive socio-economic development'.

Waziri wa Mali asili na utalii Balozi Dr Pindi Chana akizungumzia mkutano wa UNWTO-CAF) na akiwa na Naibu Waziri wa wizara yake na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela katika mkutano na waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, Waziri wa Mali asili na utalii Balozi Dr. Pindi Chana amesema kuwa maandalizi yote kuelekea mkutano huo yamekamilika na wageni Kutoka nchi mbali mbali wamekwisha wasili nchini.

Alisema kuwa Moja ya ajenda katika mkutano huo ni kujadili kuhusu mustakabali wa ustawi wa maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika hasa baada ya athari za mlipuko wa janga la uviko -19 ilivyokuwa imeathiri utalii wa kimataifa Kwa wastani wa asilimia 50 Hadi 85 katika nchi mbali mbali.

"Katika mkutat huo tutakuwa na matukio mbali mbali ikiwemo hafla ya ufunguzi, kutakiwa na zoezi la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini kupitia jukwaa la uwekezaji, lakini pia wadau wa utalii watajengewa uwezo kuhusu maswala ya masoko na zaidi kutakuwa na ziara ya mafunzo ambapo tutatumia kutangaza vivutio vilivyopo nchini"

Waziri Chana alisema kuwa Tanzania wanatarajia kutumia mkutano huo mkubwa duniani kama fursa ya kutekeleza sera ya Taifa ya kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia milioni 5 na mapato ya Dola billioni 6 ifikapo mwaka 2025.

" Mkutano huu kama nchi tutautumia Kwa manufaa makubwa kiutalii na kiuchumi katika kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan aliyeanzisha kupitia filamu yake ya 'the Royal tour' ambapo Kwa sasa tunaendelea kutanua wigo wa mazao ya utalii nchini"

Kwa Upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha aliwataka wananchi wa mkoa huu kuonyesha ukarimu Kwa wageni hao huku akiahidi kulinda ulinzi na usalama wao wote Kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

"Kikubwa wakazi wa Arusha wachangamkie fursa zitokanazo na mkutano huu Kwa watu wa hotel, migahawa, wasafirishaji na wengine pia tuendelee kulinda taswira ya mkoa na nchi Kwa ujumla Kwa kuwa wakarimu Kwa wageni bila bugha yoyote

Aidhsa Tanzani iliingia makubaliano ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo machi 7,2022 katika makao makuu ya shirika la utalii duniani nchini Uhispania iliyosainiwa na aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii,Dkt.Damas Ndumbaro na katibu wa shirika hilo Zurab Pololikashvil ambao wote watakuwa wajumbe wa mkutano wa kesho.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!