Uhasibu mabingwa wapya wa kombe la wiki ya Sheria

Arusha

 

Timu ya chuo cha uhasibu FC (IAA) imefanikiwa kutwaa kombe la michuno ya wiki ya Sheria nchini baada ya kuitandika timu ya benki ya NMB FC jumla ya mabao 3-1.

Uhasibu imetwaa kombe hilo katika bonaza la kuadhimisha wiki ya sheria nchini yaliyochezwa jana jijini Arusha katika viwanja vya General tyre.

Mahakama fc iliyokuwa na hamu ya kubeba kombe hilo,  imezimwa ndoto zake mapema katika mechi ya nusu fainali ya kwanza walipokutana na timu ya NMB baada ya kuchapwa bao 1-0 huku uhasibu fc ikikata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuichapa timu ya Benki ya CRDB fc kwa bao 2-1.

Katika bonanza hilo, timu ya uhasibu queens ilifanikiwa kufuata nyayo za vijana wao baada ya kubeba ubingwa kwa mpira wa mikono baada ya kuitandika timu ya Mahakama queens jumla ya magoli 27-26.


Katika bonanza hilo, michezo mingine iliyoshindaniwa ni pamoja na riadha mita 100 na mita 1500, sambamba na kukimbia na yai kwenye kijiko, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia kwenye magunia, bao, draft, pool table , kula na karata.



Akizungumzia mashindano hayo, Naibu msajili wa mahakama kuu kanda ya Arusha Amir Msumi amesema wameandaa bonanza hilo kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya sheria ili kutoa elimu ya maswala ya haki katika taasisi mbalimbali.

“Utoaji wa elimu pekee yake katika mfumo huo ulio rasmi tuliona kuna watu tunawakosa, hivyo tukaona ili kuwa na ushiriki na wadau wetu katika hali ya kufurahi na kushereheka ni bora siku ya kuhitimisha tukutane pia katika michezo na taasisi zingine” alisema na kuongeza;

“lengo ni tujumuike pamoja, watu wa mahakama na wadau wengine na watu wa kawaida tunaoshirikiana nao katika utoaji wa haki madai na jinai ili kufahamiana lakini pia kukuza ushirikiano maana tunaona hawa watu tunakutana nao peke yake wakija mahakani kushtaki au kusthakiwa sasa hatutaki  tena iwe hivyo” alisema Msumi.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya sheria kutoka chuo cha uhasibu Arusha ambae ni kocha wa timu hiyo amesema kuwa wamekuja kushriki mashindano hayo ili kuchangamana na watu wa sheria lakini pia kuwatoa wanafunzi na wakufunzi wao nje ya mazingira ya chuo kuchangamana na watu tofauti

“Kwanza michezo ni afya na ajira lakini hili limekuwa tofauti kwani tumekuja kukutana na watu wanaohusika na maswala ya kisheria hasa katika sekta ya utoaji haki, hivyo inasaidia kuwafahamu na kujenga nao mahusiano mazuri” amesema

Nae Kocha wa timu NMB fc, Abrahamu Mosses Mbise amesema kuwa wamefurahi kukutana katika bonanza ambalo limekuwa hamasa kwa watu wengi waliohudhuria kushuhudia michezo yao na kufanikiwa kuondoka na elimu ya maswala ya kisheria na haki zao.




Mwisho

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!