Bethy Molllel, Arusha
M’bunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Mashaka Gambo ameingilia kati sakata la Mgambo wa jiji la Arusha kuwafanyia fujo wafanyabiashara ndogondogo katika soko la Samunge na kuwanyang’anya vitu vyao.
Katika hilo Gambo ameiomba chama chake cha mapinduzi (CCM) wasifumbie macho swala hilo bali waanze kufanya uchunguzi wa kina kujua tatizo ni nini na kwanini kila kukicha migogoro haiishi katika soko hilo na watoe ushauri wa suluhu kwa serikali.
Gambo ameyasema hayo kwenye mkutano wa kuunga mkono azimio la CCM la kumteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu na Dk Hussein Mwinyi kugombea Urais kwa upande wa Zanzibar.
“Naomba niseme kuwa wale mgambo waliofanya vurugu na kunyang’anya vitu vya watu hawajatumwa na serikali ni shida zao wenyewe kwani Dk samia anawapenda wafanyabiashara nwadogowadogo na anawapenda wamachinga” amesema na kuongeza
“Na kwa sababu serikali ya CCM kazi yake ni kusimamia ilani nina uhakika chama chetu kitakwenda kukaa na kuona changamoto kubwa ni nini na serikali itaelekezwa nini cha kufanya ili wananchi wetu waendelee kubaki salama” amesema Gambo.
Tamko la Gambo linakuja baada ya hivi karibuni kuzuka vurugu kubwa katika soko la Samunge kati ya Mgambo wa jiji la wafanyabiashara wa soko hilo.
Maria Anania siku ya vurugu alisema kuwa mgmbo hao wamekuwa wakiwaonea na kuwanyang’anya bidhaa zao mara kwa mara huku wakitaka wapewe rushwa ili waachie.
“Leo tumegoma kunyang’anywa vitu vyetu na kutoa fedha zetu bure ndio maana yah ii vurugu unayoona hapa”amesema.
mwisho