Gambo afichua siri ya kura yake kwa Rais Samia

 


Bethy Molllel, Arusha

 

M’bunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Mashaka Gambo amefichua siri za kwanini amempigia kura Rais Samia ili kumpitisha kuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.

Gambo amesema amemchagua Dk Samia kuwa mgombea wa kiti cha Urais kutokana na bado ana kazi kubwa ya kuifanyia nchi hii katika sekta mbalimbali.

Gambo ameyasema hayo jana februari 1,2025 kwenye mkutano wa kuunga mkono azimio la CCM  la kumteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu na Dk Hussein Mwinyi kugombea Urais kwa upande wa Zanzibar.

“Mimi nilikuwa mmoja wa wajumbe waliopitisha jina la Rais Samia kuwa mgombea urais kwa sababu bado ana kazi ya kufanya ukizingatia maendeleo makubwa tuliyonayo yeye amekuwa Kinara wetu, sasa nani apendi maendeleo ya kuhakikisha huyu mkombozi anabaki ili tuendelee kufaidi? Amesema Gambo.

Amesema kuwa katika Jimbo lake la Arusha mjini mafanikio makubwa ya sekta ya elimu, afya, maji, kilimo na Utalii yameonekana wazi lakini pia ujenzi wa miundombinu ya barabara hasa zile zilizokuwa korofi.

“Moja maeneo yaliyokuwa na shida kubwa Arusha ni barabara lakini Rais ametuletea fedha za ujenzi wa barabara ya Sinoni, Olasiti, Kimandolu, Kaloleni hadi Mianzini na Ngaramtoni zote wakandarasi wako saiti, haya ni mafanikio makubwa ambayo hayajawahi kutokea ndio maana nikaamua kusema ndio anafaa katika uchaguzi ujao” amesema Gambo.

Mbali na hilo amesema kuwa sasa jiji la Arusha lina mitambo ya kutengeneza barabara zake za ndani tofauti na hizo ambazo zinajegwa na TARURA na Tanroad.

"Kikubwa viongozi wa Jiji hakikisheni mnasimamia vema mitambo hii ili ilete tija iliyokusudiwa

mwisho.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!