![]() |
Baadhi ya viongozi na madereva Bodaboda wakisherehekea siku ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani Arusha. |
Arusha.
Umoja wa madereva Bodaboda Mkoa wa Arusha (UBOJA) wamesherehekea siku ya mfanano wa kuzaliwa (birthday) kwa Rais Samia Suluhu Hassan leo January 27,2025 katika Ofisi za zilizoko katikati ya Jiji la Arusha.
Hafla ya sherehe hizo zilizoenda sambamba upandaji Miti, wamesema lengo ni kutambua mchango mkubwa uliofanywa na kiongozi huyo kwa chama chao.
Mwenyekiti wa UBOJA Constantine Okello amesema baadhi ya mambo makubwa iliyopelekea wao kuadhimisha sikukuu hiyo mbali na kushusha kiwango cha faini kutoka Sh30,000 hadi sh10,000 kwa makosa ya barabarani lakini pia kuwajengea Ofisi ya chama mwaka jana na kuwachangia jumla ya Sh10 milioni za kuanzisha Ushirika wa Umoja wao.