Kishindo cha NMB Bonge la Mpango, lawapa wateja wake kicheko




Mkuu wa wilaya ya Arumeru (Mwenye koti) akimkabidhi funguo ya pikipiki ya magurudumu matatu 'Guta' mfanyabishara wa mazao Issah Bakari Hassan aliyoshinda kwenye droo ya 'NMB bonge la Mpangi' jana jijini Arusha.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru (Mwenye koti) akimkabidhi  Shillah Gabriel TV yenye ukubwa wa nchi 75, aliyoshinda kwenye droo ya 'NMB bonge la Mpangi' jana jijini Arusha.

Arusha

Kampeni kabambe ya NMB bonge la Mpango imetua jijini Arusha kwa kishindo cha aina yake na kuwapa Zawadi washindi wake katika droo iliyochezwa katika viwanja vya soko la USA river wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

NMB Bonge la Mpango’ ni msimu wa nne sasa kufanyika inayokwenda na kauli ya fungua Akaunti, Weka Akiba na Ushinde ambapo kwa msimu huu mshindi wa jumla anatarajiwa kutangazwa desemba 19,2024 kwa kukabidhiwa kitita chake cha shilingi milioni 100 taslimu.

Mbali na hilo kila wiki washindi 10 wanaendelea kujinyakulia kitita cha shilingi 100,000 na vifaa mbalimbali, huku washindi wanne wa kila mwezi wakipewa shilingi milioni tano kila mmoja.

Katika soko la USA river washindi watano wamefanikiwa kucheka kwa Zawadi wakiwemo wawili waliokabidhiwa hapo hapo.

 Waliokabidhiwa zawadi ni Issa Bakari Hassan aliyekabidhiwa pikipiki ya magurudumu matatu maarufu kama ‘Guta’ na Shillah Gabriel aliyekabidhiwa TV yenye ukubwa wa nchi 75.

Mbali na hilo, droo nyingine ilichezeshwa papo hapo na washindi watatu kupatikana akiwemo Bernard Kimaro (Kahama) aliyejishindia zawadi ya power tiller, Deogratius Kisoka (Mwanza) aliyezawadiwa pikipiki ya magurudumu mawili (Toyo) na Meshack Mafie aliyezawadiwa simu janja

Meneja wa NMB kanda ya kaskazini, Baraka Ladislaus akizungumza wakati wa ugawaji zawadi na uchezeshaji wa droo ya kampeni ya 'NMB bonge la Mpango jijini Arusha jana

Akizungumzia lengo la kampeni ya Bonge la Mpango, meneja wa NMB Kanda ya kaskazini Baraka Ladislaus amesema ni kuhamasisha utamaduni wa watanzania kujiwekea akiba ili kukabiliana na dharura zinazoweza kujitokeza za uhitaji wa fedha.

Amesema kampeni hiyo ya kila mwaka ya ‘Bonge la Mpango’ inalenga kuhamasisha watu kufungua akaunti na kujiwekea akiba ili kutatua matatizo ya dharura yanayohitaji fedha ambapo mteja atajiwekea akiba ya kuanzia Shilingi 100,000 na kuendelea.

Amesema zawadi wanazotoa kwenye kampeni hiyo ya kila mwaka inayodumu kwa miezi 12 ni pamoja na kitita cha shilingi milioni 100 kila mwaka, 100,000 kila wiki, friji, TV, pikipiki ya magurudumu mawili (Toyo) na pikipiki ya magurudumu matatu (Guta na Bajaji sambamba na mashine ya kufulia,majiko ya Gesi, trekta za kilimo (Power tiller).

“Zawadi hizi tangu kuanzishwa msimu wa nne zimefanikiwa kuhamasisha watu wengi kufungua akaunti na kujiwekea akiba ambazo zimekuwa msaada mkubwa wa kuwaepusha na mikopo umiza wanapopata shida ya tatizo la kifedha” amesema Meneja huyo.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Amiri Mkalipa akizungumza wakati wa ugawaji zawadi na uchezeshaji wa droo ya kampeni ya 'NMB bonge la Mpango jijini Arusha jana

 

Akizungumzia kampeni hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Amiri Mkalipa amesema kuwa kampeni hiyo ni muhimu kwa wananchi wote hasa wafanyabiashara ambao wamekuwa na dharura ya kifedha mara kwa mara hivyo kuwataka kuchangamkia fursa hiyo.

Pia aliwataka NMB kutembea mara kwa mara kwa wananchi walioko pembezoni wakiwemo wakulima katika wilaya yake ambao wamekuwa wakipata changamoto za kifedha mara kwa mara lakini kukutana na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu na kuwaingiza kwenye mikopo umiza.

Akizungumzia zawadi aliyoshinda, Hassan amesema kuwa Guta hiyo itamsaidia katika usafirishaji wa bidhaa zake za nafaka ambazo amekuwa akitumia gharama kubwa kufikisha katika kituo cha biashara kutokana na kukodisha usafiri.

“Nashukuru sana NMB, kwa sasa nina usafiri wangu sio mchana wala usiku niko huru kuhamisha nafaka zangu katika minada mbalimbali bila kujali gharama, tofauti na mwanzo nilikuwa napoteza zaidi ya 150,000 hadi 200,000 kwa usafiri pekee wa kuzunguka katika minada kufuata wateja na kufanya faida yangu kuwa ndogo” amesema.

 


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!