Muhimbili walivyorejesha tabasamu la mtoto Maliki aliyechinjwa na msichana wa kazi

 

Hatimae tabasamu limerejea usoni mwa mtoto Maliki Hashimu, mkazi wa Goba Jijini Dar es Salaam, baada ya afya yake kuimarika na kuruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea na majukumu yake ikiwemo kwenda shule.

Mtoto Maliki ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kuonekana afya yake imeimarika baada ya kupata matibabu  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Maliki alikuwa alikuwa akipatiwa matibabu MNH kutokana na majeraha makubwa aliyopata baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mfanyakazi wa ndani ‘house girl’, julai 15,2024.

Jeraha hilo lilisababisha kutenganisha njia ya hewa chini ya sanduku la sauti na kusababisha ashindwe kupumua, kuongea, na kumpatia maumivu na kupoteza damu nyingi.



Akielezea furaha yake, mama mzazi wa Maliki ameishukuru serikali kwa kumsaidia juu ya matibabu ya mwanae.

"Siwezi hata kuelezea furaha ya mwanangu, kiukweli nimejisikoa furaha sana, Namshukuru Rais wetu mama Samia na viongozi wote kwa ujumla na madaktari kumsaidia mtoto wangu ambae nilikwisha kata tamaa kama anaweza kuishi tena" amesema.

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk. Rachel Mhavile amesema watalaam wa hospitali wamejiridhisha juu ya afya ya mtoto huyo baada ya uangalizi na matibabu ya mda mrefu na wanamruhusu rasmi.

"Kulingana na huduma alizopata mtoto huyo tangu alipopokelewa tarehe 15 Julai mwaka huu, tumeridhika na afya yake na sasa yupo salama hivyo tunamruhusu aende nyumbani ili kuendelea na shule na maisha yake ya kawaida huku hospitali tukiendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo yake huko" amesema Mhavile.




Naye Daktari Bingwa wa Tiba na Magonjwa ya Dharura, Dk. Juma Mfinanga amesema kutokana na hali mbaya aliyokuja nayo mtoto huyo julai 15,2024 waliharakisha huduma za awali ikiwemo kurejesha hali ya upumuaji na kupata damu.

 " Baada ya hapo tuliita timu husika ya wabobezi wa upasuaji wa shingo, pua, koo na masikio na wao wakafanya kazi yao kwa umahiri mkubwa ndio yakaleta mafanikio haya Leo" amesema.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post