![]() |
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo |
Arusha
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia Dominick Miduriek (32) mkazi wa Oldonyokumur kata ya Muriet jijini Arusha kwa tuhuma za kumwingilia kijana wa miaka (23) kinyume na maumbile.
Dominick ametekeleza uhalifu huo Ili kuficha aibu ya kuomba kuingiliwa kinyume na maumbile na kijana huyo na kukataa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo amesema kuwa Jeshi lake Bado linafuatilia tukio hilo.
"Hilo tukio nimesikia tu juu juu, ngoja Askari wangu wanafuatilia tukio hilo na tutakachofanikiwa ntakujulisha zaidi" amesema Masejo.
Akisimulia tukio hilo, Kijana huyo amesema kuwa usiku wa Jumatatu Julai 22,2024 majira ya saa Tano usiku alikuja mtuhumiwa na kumgongea mlango wake huku akimwomba kumsaidia kusukuma pikipiki yake kuelekea nyumbani kwao.
"Huyu mtu anaishi Mtaa wa pili, akaja Kumuomba nikamsaidie kusukuma pikipiki yake hadi nyumbani kwao kwa madai kuwa anaogopa kuiwasha itatoa mngurumo ambao mama yake wanaoishi nae atasikia na kumgombeza kuwa anatoka wapi usiku huo" amesema kijana huyo.
Bila kujua dhamira ya mtuhumiwa, Kijana anasema kuwa ilibidi atoke Ili kwenda kumsaidia, hivyo wakaongozana kuifuata pikipiki iliyokuwa pembeni ya nyumba mpya ya mtuhumiwa lakini haikuisha, hivyo alikuwa anaishi upande wa pili wa nyumba nyingine.
"Ni kama kilomita moja kutoka kwao na kwetu na hiyo nyumba yake anayojenga Iko mita chache karibu na kwao, hivyo tulivyoifikia pikipiki yake nataka kusukuma akaniambia subiri kwanza usisukume, njoo nisaidie kuhesabu hizi hela zangu nimepewa kwenye kikoba Ili nigawanye kwenye mifuko isipotee ntakugaia" amesema kijana huyo.
Amesema kuwa baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo ambayo haikuisha, mtuhumiwa alifunga mlango wa grili kwa kufuli kwa madai wasivamiwe na alitandika mifuko iliyokuwa pembeni ya ukuta na kutoa hela kuanza kuhesabu kabla ya kuvua nguo na kuhitaji kuingiliwa.
"Nimeingia tu akasema ngoja nifunge mlango tusivamiwe, nikashangaa ametoa kufuli na kufunga mlango, kisha akatoa pesa tukahesabu kiasi cha laki tatu na themanini akaweka pembeni akavua nguo akaniambia anahitaji nimwingilie"
"Nilishtushwa na jambo hilo sana, nikakataa nikaanza Kumuomba msamaha kwa kuwa Mimi ni kiongozi wa vijana Kanisani, lakini alizidi kunitisha tena akavunja moja ya chupa iliyokuwa kwenye nyumba hiyo na kunitishia kuniua, lakini pia sikukubali. Amesema.
Amesema kuwa baada ya mvutano mkubwa huku wakipambana alimzidi ngumu na kufanikiwa kumvua koti na suruali aliyokuwa amevaa na kufumnga nayo mikono na miguu kabla ya kumuingilia.
"Baada ya mparangano wa mda mrefu, aliniambia 'sasa wewe utaniaibisha kwa kwenda kunitangaza Mimi ni wa michezo hii hivyo ili isiwe hivyo nakufunga mdomo kwa kukuingilia wewe', ndio akanigeuza na kunifanya kwa nyuma akiwa amenifunga na suruali hadi alipomaliza" alisema kijana huyo.
Akizungumzia tukio hilo, baba mkubwa Mathayo Mollel amesema kuwa mtuhumiwa huyo mwenye mke na watoto wawili ameidhalilisha kabila la kimasai ambao ni mkosi mkubwa hata kushikwa tu na mwanaume mwenzio sehemu za makalio licha ya kuingiliwa.
"Hii ni aibu na mkosi mkubwa hata kumshika tu mwenzio makalio yake licha ya kumuingilia, kiukweli ametutia gundu kubwa tunaomba serikali itusaidie kumuadhibu mtu huyu"amesema Mollel.
Amesema kuwa katika kutaka kuziba tukio hilo, mtuhumiwa akishirikiana na mama yake wametuma wazee kuleta ng'ombe , kondoo na kreti mbili za soda kuomba msamaha kimila lakini kwa udhalilishaji huo wamegomea zaidi wanaiomba serikali kuchukua hatua Kali dhidi ya kijana huyo Ili kunusuru kizazi kueneza matukio hayo.
Mjomba wa kijana mwathirika wa ulawiti, Leaky Satiani Amesema kuwa kwa sasa kijana huyo amedhurika vibaya ikiwemo kutoka kinyesi bila kujizuia
.