Wazee wataka kutibiwa tezi dume kwa bima za afya

 

mwenyekiti wa umoja wa wazee waishio jiji la Arusha, Isihaka Kivuyo (kulia) akipokea  hati ya usajili Kutoka kwa mwakilishi wa m'bunge wa Arusha mjini, Mrisho Gambo, afisa maendeleo ya jamii jiji la Arusha, Ahadi Msangi 

Bertha Mollel - Arusha


Umoja wa wazee waishio jiji la Arusha wameiomba serikali itazame upya uwezekano wa kuongeza huduma zitolewazo kwenye bima za afya kwani haikidhi mahitaji yao.


Wazee hao wamesema kuwa huduma zilizoko kwenye bima za afya zitolewazo haikidhi mahitaji yao Kwani haitibu magonjwa yale makubwa yanayowasumbua ikiwemo tezi dume na presha.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa umoja wa wazee waishio jiji la Arusha, Isihaka Kivuyo wakati wa uzinduzi rasmi wa umoja wao uliokwenda sambamba na kukabidhiwa hati ya uhalali wa kujiendesha.

"Yako maradhi ambayo yanawasibu wazee kutokana na kupungua Kwa kinga ya mwili na nguvu ambayo yamekuwa chanzo kikubwa Cha vifo vyao na bahati mbaya wengi hawamudu  gharama za matibabu kwani ni kubwa" alisema Kivuyo na kuongeza...

"Tunaomba  serikali itusaidie kuzipitia upya vifurushi vya bima za afya na kuhakikisha inatibu maradhi makubwa yanayowasumbua wazee ikiwemo tezi dume, kisukari, Kansa, presha, lishe na miguu"




Alisema kuwa lengo kubwa la umoja huo ni kuona namna wazee Wanavyoweza kusaidiana katika matatizo mbali mbali na kupaza sauti Kwa umoja wao waweze kusaidika.

"Lengo letu sio kuwa omba omba bali tumeungana kuhakikisha tunapaza sauti lakini kuona fursa zilizoko kwenye jamii na serikali yetu na kuzitumia Kwa manufaa yetu na taifa kwa ujumla kiuchumi, kijamii na kisiasa"

Akimuwakilisha m'bunge wa Arusha mjini, Mrisho Gambo, afisa maendeleo ya jamii jiji la Arusha, Ahadi Msangi aliwataka wazee hao kuheshimu umoja wao na kuitunza kwani utawaletea manufaa na heshima kubwa.

"Lakini pia hizi siku wazee mmejisahau majukumu yenu kwenye jamii ya kutunza maadili na kukemea kuporomoka kwa Mila, desturi na tamaduni zetu, hali hiyo imeibua matukio mengi ya ukatili, ubakaji na ulawiti kwenye jamii.. naomba mrudi upya kazini mkayatekeleze hayo"

Akizungumza na wazee wenzake, Philemon Kisamo aliwataka wenzake kutokubweteka majumbani wakisingizia umri mkubwa badala yake wajishughulishe na kazi mbali mbali za kiujasiriamali hasa kilimo kidogo na ufugaji.

"Kuwa mzee sio ndio umeisha kila kitu, baadhi ya maradhi tunayataka wenyewe, niombe wazee wenzangu tusiwe mzigo Kwa familia na jamii inayotuzunguka Kwa kuwa omba omba bali tujifanyie shughuli za kujiingizia kipato kama kilimo Cha mboga mboga na matunda hata ufugaji wa mifugo tofauti na kuku"


Kwa upande wake mmoja wa wazee hao Jenifer Shoo aliiomba serikali kuwatengea fungu la angalau asilimia 1 ya mikopo inayotolewa na halmashauri kama wanavyotoa Kwa vijana, wanawake na walemavu Ili kuwasaidia kuendesha miradi midogo midogo ya nyumbani wasiwe tegemezi.



Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!