Dr Mpango kufungua mkutano wa mabaraza ya Habari Afrika

 


Arusha

 Makamu wa Rais Dk Philip Mpango, anatarajia kufungua mkutano wa pili wa mabaraza ya Habari Afrika 2025, unaotarajia kufanyika kwa siku tatu jijini Arusha.

Mkutano huo ulioandaliwa na Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA) kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania (MCT) utaanza Julai 14 hadi 17,2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (Aicc), kwa kukutanisha zaidi ya washiriki 500 kutoka Mataifa 19 wanachama wa umoja huo.


Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Arusha, Mwenyekiti wa NIMCA, Ernest Sungura, amesema mkutano huo una lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha uhuru na uwajibikaji wa vyombo vya habari barani Afrika.

 “Mkutano huu utakaofunguliwa na Dk Mpango utaongozwa na kauli mbiu isemayo “Uboreshajji usimamizi wa vyombo ya habari na mawasiliano ni msingi wa weledi wa uandishi wa habari”amesema Sungura ambae pia ni Katibu Mtendaji wa MCT.

Sungura amewataja miongoni mwa wageni maalum watakaohudhuria mkutano huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Dk Tawfik Jelassi na Mawaziri wa Habari wa Kenya, Uganda, Zambia na Nigeria. 

“Katika mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo matumizi ya akili mnemba na masuala ya kijinsia na ulemavu yanavyopaswa kupewa kipaumbele”.

Amesema kuwa watatumia mkutano huo pia kuadhimisha miaka 30 ya tangu kuanzishwa kwa Baraza la Habari Tanzania na kuangazia mafanikinikio na changamoto zake.

“Mbali na kuweka mikakati ya kuimarisha uhuru na uwajibikaji wa vyombo vya habari barani Afrika, Mkutano huu pia tunatarajia kuwa jukwaa muhimu la kukuza ushirikiano wa kitaasisi na kubadilishana uzoefu” amesema.

Nae mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) Abraham Gwandu amesema kuwa wanatarajia kujifunza mengi kutoka kwa waandishi wa mataifa mengine kwa ajili ya kukuza uhuru wa vyombo vya habari nchini na haki na wananchi kupata habari.

Mwisho…

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!