MKURABITA waiongezea mapato halmashauri ya jiji la Arusha.

 



Bertha Mollel, Arusha.


 Mpango wa Kurasimisha rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA) imefanikiwa kuiongezea mapato halmashauri ya jiji la Arusha kupitia lesseni za biashara kutoka bilioni 1.440 hadi bilioni 3.165.

 

Hayo yamebainishwa na kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha, Hargeney  Chitukuro wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo jumuishi cha urasimishaji na uendelezaji wa biashara katika halmashauri ya jiji la Arusha, mbele ya waziri wa nchi, ofisi ya Rais menejimenti  ya utumishi wa umma na utawala bora Jenister Mhagama.

 

Chitukuro alisema kuwa kabla ya ujenzi wa kituo hicho walikuwa wanakusanya billion 1.440 lakini tangu serikali kuwaletea waraka kupitia ofisi ya MKURABITA mwezi agost 19, 2020 ya  kuwataka waanzishe kituo hicho walifanikiwa kukamilisha ujenzi mwaka 2021 na kuanza kazi rasmi mwezi march ambapo hadi septemba 2022 wamefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni  3.165 zilizotokana na ada za leseni za biashara zilizorasimishwa.

 

“Kwa kutumia mfumo huu wa kituo jumuishi halmashauri imefanikiwa kukusanya fedha hizo kwenye jumla ya biashara 6,159 zilizorasimishwa, matunda hayo yameletwa na uwepo wa kituo hiki ambacho kimewarahisishia wafanyabiashara kupata huduma za mahitaji yao yote mahali pamoja ikiwemo ushauri wa kibiashara hali ambayo pia imepunguza urasimu wa utoaji huduma”

Alisema kuwa kituo hicho kinasimamiwa na halmashauri ya jiji la Arusha kupitia divisheni ya viwanda , biashara na uwekezaji  na kitakuwa na wadau wahusika wakiwemo mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA’, brela, SIDO, polis, uhamiaji, watoa huduma za kifedha kama mabenki lakini pia watu wa bima za afya na watoa fursa za viwanda vidogo.

Kwa upande wake Waziri Mhagama aliipongeza halmashauri ya jiji la Arusha kujenga kituo hicho huku akiwataka kuhakikisha wafanyabiashara wanapata huduma stahiki ili waweze kuongeza pato lao na taifa kwa ujumla.

Pia aliwataka wafanyabiashara kutumia vyema kituo hicho katika uendelezaji wa biashara zao  ili waweze kuziongezea thamani kupitia mafunzo yatakayotolewa mara kwa mara lakini pia fursa za huduma zingine ikiwemo fedha zinazotolewa  na halmashauri na taasisi za kifedha kwa njia ya mikopo ya uwezeshaji.

 

“Niombe watendaji katika kituo hichi muweke mpango mzuri wa urasimishaji usio na usumbufu wowote kwa wafanyabiashara wanaokuja kupata huduma hapa kwani bila kufanya hivyo utakiondolea kituo hiki thamani lakini pia kuvuruga mpango mzima wa serikali wa kuwapa nguvu ya kiuchumi wananchi kwa kuwaongezea uwezo wa kumiliki na kufanya biashara katika mfumo rasmi unaozingatia utawala wa sheria.

“lakini niwageukie na nyie maafisa wa MKURABITA, mnapaswa kuongeza jitihada za kuwaelimisha wafanyabiashara faida ya kurasimisha biashara pamoja na namna bora ya uendelezaji wa biashara zao kwa manufaa ya kila mmoja”

 

Kwa upande wake mmoja wa wafanya biashara wa jiji la Arusha Athumani Kikoi alisema kuwa kituo hicho kitawasaidia katika kuokoa mda wa kuzunguza katika ofisi mbali mbali kwa ajili ya kurasimisha biashara zao hivyo kuiomba serikali kuboresha mfumo wa utoaji huduma hasa zinazotegemea mtandao.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!