Wahasibu wakuu Afrika kukutana Tanzania kujadili usalama wa fedha za Serikali.

 Mhasibu Mkuu wa serikali (CPA) Leonard Mkude 


Arusha. Zaidi ya Wataalamu wa fedha 2000 kutoka nchi zote 55 za Afrika wanatarajia kukutana jijini Arusha kujadiliana maswala ya mbalimbali ya kihasibu, ukaguzi na Usalama wa fedha katika serikali za nchi za Afrika.

Lengo ni kubadilishana uzoefu wa upatikanaji wa fedha, matumizi na Suluhu la changamoto zake ikiwemo mifumo ya kidigiti kwa hatma ya maendeleo ya wananchi waliopo sasa na vizazi vijavyo.


Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari juu ya mkutano huo, mhasibu mkuu wa serikali (CPA) Leonard Mkude amesema Mkutano huo wa pili wa wahasibu barani Afrika (AAAG) utafanyikia kwa siku tatu kuanzia Desemba 2 hadi 5 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa AICC.

"Mkutano huu utashirikisha wataalam wote wa fedha wakiwemo wahasibu wakuu,wakaguzi wa hesabu na wahusika wa Tehama walioajiriwa kwenye taasisi za umma,kampuni na sekta binafsi"amesema Mkude.

Amesema kuwa, katika mada hizo watabadilishana uzoefu juu ya mifumo ya usimamizi wa fedha za umma, pia watajadili changamoto na Suluhu za maswala ya kifedha kwa uthabiti wa kiuchumi (strong economy).


Mwenyekiti wa AAAG, Malehlohonolo Mahase, 


Mwenyekiti wa AAAG, Malehlohonolo Mahase, amesema maandalizi ya mkutano huo wa kimataifa yanaendelea ambapo  mbali na wataalam wa fedha Afrika pia wamealikana wadau wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia, Shirika la Global Fund na Shirika la Fedha duniani (IMF) watashiriki kikao hicho.

Amesema kupitia mkutano huo watasisitiza nchi wanachama kukusanya kodi kwa lengo la kuhudumia wananchi ipasavyo pamoja na kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa kuzingatia matumizi sahihi ya rasilimali fedha na kuwa wawazi kwa jamii. 

"Tumeamua kufanyia mkutano huo Tanzania kutokana na ni miongoni mwa nchi vinara katika matumizi ya mifumo ya kibajeti hivyo tunaamini tutajifunza, lakini pia kuwa nchi yenye Amani na demokrasia njema"amesema.

Amesema kuwa wawapo hapa nchini pia wataweza kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji  ikiwemo sekta ya utalii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Christine Mwakatobe


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Christine Mwakatobe, amesema kituo hicho kimejipanga kutoa huduma bora kwa washiriki wa mkutano.

"Kufanya kwetu vizuri kwenye mikutano kunakuza hata utalii wetu na kuongeza fedha za kigeni "

Mwisho

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post