Mawakala wa Hispania wapigana vikumbo kusaka vipaji Mashindano ya Chipkizi cup Arusha



Bertha Mollel - Arusha.

 Jumla ya timu 302 kutoka nchi za Afrika zimetua jijini Arusha kushiriki Mashindano maalum ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, yaliyoanza jana jijini Arusha katika viwanja mbali mbalimbali.

Katika Mashindano hayo, taasisi mbali mbali zimetuma mawakala wao kwa ajili ya kusaka vipaji huku wawakilishi kutoka ligi kuu ya Hispania (Laliga) na Taasisi ya kukuza vipaji vya soka Hispania (SFI) vikipigana vikumbo zaidi katika kuwania mawasiliano ya Chipkizi hao.

Mashindano hayo yanayoshirikisha timu za soka la vijana chini ya umri wa miaka saba, tisa, 11, 13, 15, 17, na 20 Kwa wanaume na wanawake zimetoka mikoa mbali mbali za nchi za Afrika mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi.

Nchi zingine zilizoleta timu ni kutoka Somalia, Cameroon, Zimbabwe na Nigeria.

Akizungumzia uwepo wao, Mkurugenzi wa Taasisi ya Soka ya Uhispania (SFI) Pablo Verdejo alisema kuwa wamehudhuria Kombe la Chipkizi, Ili kusajili wachezaji wapya ambao watachukuliwa kwa udhamini maalum ili kuwafanyia majaribio ya michezo nchini Hispania.



"Tuko hapa kupata mawazo na uzoefu zaidi ya uendeshaji wa mashindano ya vijana lakini pia kuelezea jinsi tunavyofanya kazi nchini Uhispania, lakini zaidi tumekuja kutafuta wachezaji wazuri tutakaowachukua Kwa majaribio kwetu na kama wakionyesha uwezo zaidi watapata nafasi ya kusajiliwa kwenye kituo chetu na kuendelezwa vipaji vyao Kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa


Akizungumzia Mashindano hayo, Alfred Itaeli ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Future Stars Academy (FSA), inayoandaa Mashindano hayo ya Soka ya Vijana Afrika Mashariki, amesema timu 302 zimeshiriki.

"Lengo la Mashindano haya ni kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao Ili kupata nafasi ya kuendelezwa hivyo tunafurahi kuona mawakala wengi zaidi wapo hapa kutoka nchi mbali mbali na wengine kutoka hapa nchini"



Nae mwakilishi wa TFF, mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha, Zakayo Mjema alisema wanafurahi vijana kupata jukwaa Hiloa kuonyesha vipaji ambapo wao wanatumia kuhakikisha wanawaona vijana wazuri wa kitanzania watakaotumika katika timu zetu za Taifa.

Katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo, ilishuhudiwa timu ya Future star ikianza vema Mashindano hayo baada ya kuwafunga timu ya Nshupu jumla ya mabao 4 -2 katika uwanja wa TGT.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!