Balozi
Njoolay, Sabaya waongoza mamia kumzika Mzee Kitimu
Bertha Mollel - Arusha.
Aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria na mkuu wa mkoa wa Arusha, Daniel ole Njoolay, pamoja na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Serengeti, Thomas Sabaya wameongoza mamia ya wananchi wa wilaya ya Arumeru kumzika aliyekuwa diwani wa kata ya Olturment Reuben Elias Kitimu, aliyefariki agost 26 mwaka huu katika kituo Cha matibabu Cha Arusha Lutheran (ALMC).
Kitimu aliyekuwa pia daktari bingwa wa mionzi katika hospital ya Seliani Lutheran, amefariki akiwa na miaka 86 baada ya kuugua kwa mda mrefu, ambapo Jana amezikwa katika makaburi ya kifamilia yaliyoko nyumbani kwake Olturment.
Akitoa Salam
za pole kwa familia, aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria Daniel ole
Njoolay amesema kuwa amemfahamu marehemu tangu akiwa mkuu wa mkoa wa Arusha
mwaka 1995 katika harakati zake za kitabibu lakini zaidi akiwa mwanachama
mtiifu wa TANU.
"Hakika
tumepoteza mtu muhimu sana kwani mbali na kupigania maisha ya watu, na chama
chake Cha TANU kabla ya kuwa CCM, lakini pia ameshiriki kupigania nchi enzi ya
vita ya Kagera akiwa mmoja wa wanajeshi
waliosimama imara kuhakikisha Tanzania haipokwi hata MITA Moja na
waasi" amesema Balozi Njooolai
Njoolay
alisema kuwa kupigania maslahi ya maendeleo ya wananchi wake, uzalengo na vita
dhidi ya rushwa vilimfanya Kitimu kuwa maarufu zaidi ambapo amewataka madiwani
wengine kuiga mfano huo ili kuepuka migogoro yasio na manufaa.
"Mimi
binafsi nilifarijika sana baada ya nchi kuitambua eneo la Olturment kama kata,
Kitimu alipata nafasi ya kuwa diwani wa kwanza kusimamia shughuli zote
kuhakikisha eneo hili linakuwa na hadhi ya kata Kwa kuleta maendeleo makubwa
ikiwemo ujenzi wa hospital na shule"
Kwa upande
wake aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Serengeti na Songea, Thomas Sabaya alisema
urafiki wake na Mzee Kitimu ulianzia tangu wakiwa vijana hadi kushindana katika
kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya chama ikiwemo uwenyekiti wa
halmashauri ya Meru.
"Nitazidi
kumuenzi rafiki yangu maana amenionyesha njia salama ya siasa katika mapito
yote tuliyopita, aliipenda chama tangu TANU na hata ilipokuja kuwa CCM
aliipenda zaidi na kuwa tiyari kutumika mda wote" alisema Sabaya ambae ni
baba mzazi wa Lengai aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai.
Kwa upande
wake Mtoto wa marehemu, Dr. Shedrack Kitimu, ambae ni mhadhiri chuo kikuu
SUA, alisema kuwa baba yake alianza
kuugua ugonjwa wa kiharusi ya ubongo mwaka 2020 na kujaribu kutibiwa katika
hospital mbali mbali nchini huku alipata nafuu na kuzidiwa tena hadi kifo.
"Baba
yetu alizaliwa November 1936 hapa Arusha ambapo kabla ya kifo chake alihudumu
katika hospital mbali mbali za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Singida na Tanga
kama mtaalamu wa mionzi huku akishika nyadhfa mbali mbali katika chama tangu
ikiwa TANU hadi kuwa diwani wa kwanza wa CCM kata ya Olturment"
Akizungumza
Katika ibada ya mazishi hayo, Naibu katibu mkuu Misioni na uinjilisti, dayosisi
ya kaskazini kati, mchungaji Laretoni Loishiye alisema kuwa kiburi, majivuno na
dharau zimekuwa chanzo Cha kinachopelekea binadamu kushindwa kufikisha umri wa
miaka 70 iliyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu.
"Hayo yote ni maovu yanayopelekea hata matukio ya ukatili, unyanyasaji baina yetu na hata mauaji.., tufuate njia ambazo zimekuwa mfano kwa baadhi ya waasisi wetu waliozaliwa miaka ya nyuma hakika wengi wao wanaishi maisha marehem