Na SAID MWISHEHE
Shaka
akiwa katika ziara hiyo iliyoanza jana visiwani humo amepata nafasi ya
kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa na kisima cha maji safi na salama
katika Jimbo la Gando, miradi ambayo imewapunguzia adha wananchi ikiwemo
ya kufuata maji umbali mrefu.
Akiwa
katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Salim
Mussa Omar na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mariam Thani Juma na kufanyika
kwenye Uwanja wa Mpira Kizimbami Shaka amesema utekelezaji wa miradi ya
maendeleo unaofanyika katika jimbo hilo na maeneo mengine yanayoongozwa
na wabunge na madiwani wa CCM.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu
Shaka akionesha jambo alipokuwa akikagua moja ya mradi ujenzi wa Vyumba
sita vya madarasa ulioanzishwa na Wananchi wenyewe kwa kutoa michango
ya fedha na nguvu,sambamba na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na kamati
ya maendeleo ya Shehia ya Gando,ndani ya jimbo la Gando.
Mbunge
jimbo la Gando Mhe.Salim Mussa Omari akizungumza jambo mbele ya Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu
Shaka katika kijiji cha Raha jimboni humo. Ndugu Shaga alikagua mradi
huo wa Kisima cha Maji na kushiriki ujenzi wake.
KATIBU
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu
Shaka amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo visiwani
Pemba huku akitumia nafasi hiyo kueleza Chama hicho kitaendelea
kuwalinda na kutambua mchango wa wabunge,madiwani na wawakilishi ambao
wako mstari wa mbele kutekeleza miradi ya maendeleo.


Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu
Shaka (wa pili kulia) akikabidhi funguo ya gari la kubebea wagonjwa kwa
mmoja ya wananchi wa Jimbo la Gando (wa pili kushoto). Shaka amekabidhi
funguo za gari hilo jana likiwa limetolewa na Mbunge wa Jimbo la Gando,
Salim Mussa Omari (wa kwanza kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa.
"Utekelezaji
wa miradi unaofanywa na viongozi wa CCM unalenga kutekeleza ahadi na
kutatua changamoto za wananchi katika huduma za jamii ikiwemo afya,
elimu na maji.Niwahakikishie wabunge,madiwani na wawakilishi wanaotokana
na CCM kwamba Chama kitaendelea kuwalinda dhidi ya yeyote anayetaka
kuwavuruga na kusababisha washindwe kutekeleza majukumu yao.

"Wabunge,madiwani
na Wawakilishi wanapaswa kuachwa watekeleze Ilani ya Uchaguzi ya CCM na
kwamba mwanachama yeyote mwenye malengo ya kuomba uongozi asubiri
wakati mwafaka unaoruhusiwa kisheria,"amesema Shaka .
Maelezo
hayo ya Shaka yalitokana na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Gando
kutoa kilio chao mbele ya mkutano huo kuna baadhi ya wanachama wa Chama
chao wamekuwa wakiwashika mashati na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi Mkuu pamoja na miradi ya maendeleo,hivyo kutoa ombi
kwa Chama kuangalia namna ya kukomesha hali hiyo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu
Shaka (katikati) akisalimiana na Mwananchi wa jimbo la Gando vsiwani
Pemba baada ya kumkabidhi baiskeli ya Kutembelea iliyotolewa na Mbunge
wa jimbo hilo Salim Mussa Omari (wa pili kulia). Shaka amemkabidhi
baiskeli hiyo jana na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba
Mberwa Hamad Mberwa.
Awali
kabla ya kuhudhuria mkutano huo mapema asubuhi aada ya kuwasili
kisiwani Pemba , Shaka alizuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Tatu
marehemu Dk. Omari Ali Juma, wilayani Chakechake.
Shaka
baadae alikwenda kwenye kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais
Zanzibar marehemu Maalim Seif Sharif Hamad lililopo Kijiji cha Mnyali,
Mtambwe wilaya ya Were Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akiwa
katika makaburi hayo Shaka ametumia nafasi hiyo kueleza mchango wa
viongozi hao ambao enzi za uhai wao wamelitumikia Taifa kwa uadilifu
mkubwa na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na uzalendo mkubwa.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu
Shaka akiwa sambamba na Mbunge jimbo la Gando Mhe.Salim Mussa Omari (wa
pili kulia) akishiriki ujenzi wa kisima cha maji safi na salama katika
Jimbo la Gando, miradi ambayo imewapunguzia adha wananchi ikiwemo ya
kufuata maji umbali mrefu.
Aidha
amesema wakati Watanzania wakiwa wametimiza miaka 30 ya mfumo wa vyama
vingi vya siasa mchango wa Dk .Omari Ali Juma pamoja na Maalim Seif
hautasahaulika kwani walijitoa kwa kiwango kikubwa kuufanikinisha mfumo
huo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu
Shaka akishiriki ujenzi wa kisima cha maji safi na salama katika Jimbo
la Gando, miradi ambayo imewapunguzia adha wananchi ikiwemo ya kufuata
maji umbali mrefu.