chipukizi wa kuogelea washindana leo Dar-es-salaam

 

  

……………………..

Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam

Jumla ya waogeleaji 200 chipukizi kutoka klabu tisa za mchezo  leo Jumamosi Julai 2 wataanza kushindania medali na vikombe katika mashindano yatakayofanyika kwenue bwawa la kuogelewa la shule ya sekondari ya Shaaban Robert ya jijini.

Mashindano hayo ya siku mbili, yameandaliwa na Chama cha Kuogelea Cha Tanzania (TSA) chini ya mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Hadija Shebe. Hadija amezitaja timu ambazo leo zitaanza kuwania taji hilo kuwa ni  Bluefins, Champion Rise, FK Blue Marlins, Lake swimming club, MIS Piranhas, Mwanza Swim Club, Pigec, Dar es Salaam Swimming Club na Taliss-IST .

Alisema kuwa timu hizo zimekuwa katika maanalizi makali kwa takribani mwezi mmoja na wanatarajia kuwa na ushindani mkubwa kutoka kila klabu na muogeleaji.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Kilombero Sugar Company Limited  ambao ndiyo wadhamini wakuu  huku Burger 53, Rap & Roll, Pepsi na F & L Juice ni wadhamini wasaidizi.

Kwa mujibu wa Hadija, mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji chipukizi kuanzia miaka 12 kushuka chini na yana lengo la kuibua vipaji vya waogeleaji  kwa ajili ya kushiriki mashindano makubwa na ya kimataifa.

 “Mashindano haya yatatoa fursa kwa waogeleaji ambao walishindwa kushindana katika mashindano ya wakubwa kutokana na kigezo cha umri, kwa vile TSA inatambua waogeleaji chipukizi, tumeamua kuandaa mashindano ambao yatawafanya  waogeleaji wanaochipukia nao kujipima uwezo wao,”alisema.

Alisema kuwa kutakuwa na makundi manne, kundi la waogeleaji waliochini ya miaka saba, waogeleaji wa miaka nane na tisa, 10 na 11 na 12. Washindi wa jumla katika kila kundi atazawadiwa kikombe wakati washindi wa kila shindano watapata medali.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!