NA Mwandishi wetu.

KLABU ya Azam FC imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao baada ya kumsajili Mfungaji Bora wa Azam Sports Federation Cup (ASFC), Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ kutoka Coastal Union kwa mkataba wa miaka mitatu.

Sopu ambae mabosi wake wa zamani Simba SC walianza kumnyatia kuitaka saini yake kwa mazungumzo ya Siri Siri, Yanga nao walionekana kumsumbua usiku kucha katika kambi waliyokuwa wamefikia jijini Arusha Mara baada ya mchezo wa fainali wa kombe la Azam.

Katika mchezo huo licha ya coastal union kushindwa kutwaa kombe lakini Sopu alionekana kuwasumbua vigogo- hao wa soka dakika 120 zote walizocheza Hadi kuwapeleka hatua ya matuta.

Sopu anakuwa mchezaji mpya wa nne na wa pili tu mzawa, baada ya kiungo mshambuliaji, Cleophace Mkandala kutoka Dodoma Jiji pamoja na wageni watatu, viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho kutoka Ivory Coast na kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala.

Usajili wa safari hii ukifanywa na mmiliki wa timu mwenyewe, Yussuf Bakhresa kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu, Abdukkarim Amin (Popat). 
Azam FC imeimarisha benchi la ufundi kwa kumrejesha aliyewahi kuwa mchezaji na kocha wake Msaidizi, Kali Ongala safari hii akipewa jukumu la kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili.

 kocha mpya wa makipa, raia wa Hispania, Dani Cadena ambaye amewahi kufundisha klabu za Sevilla na Real Betis za Hispania na nyingine za China na Asaudi Arabia akiwa na uzoefu mkubwa na elimu ya juu ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA).