KATIBU MKUU MSAIDIZI WA UMOJA WA MATAIFA KUFANYA ZIARA TANZANIA


 

Na.Catherine Sungura,WAF-Dodoma


Katibu Mkuu Msaidizi na Mratibu Mkuu wa Kimataifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka Umoja wa Mataifa Dkt. Ted Chaiban anatarajia kuja nchini Tanzania mwanzoni mwa mwezi Julai 2022


Akizungumza na Waziri wa Afya Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini Tanzania   Dkt.Zabulon Yoti amesema  kuwa Kiongozi huyo anatarajia kuwasili nchini kwa ziara ya siku nne kuanzia  tarehe 4 hadi 7 mwezi ujao ambapo atapata nafasi ya kutembekea Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Dodoma


Amesema lengo la ziara hiyo hapa nchini ni kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na masuala mengine ya Afya.


Wizara ya Afya hivi karibuni ilizindua kampeni ya Global Vax Initiatives yenye lengo  la kuhamasisha jamii kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na kufuatilia wale ambao hawakukamilisha chanjo zenye dozi mbili.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!