Chipukizi wa Azam aula Ubelgiji

 


KIUNGO chipukizi wa Azam, Mtanzania Novatus Dismas Miroshi amejiunga na klabu ya SV Zulte Waregem ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Miroshi amesaini mkataba wa kujiunga na SV Zulte Waregem jana, akitokea Beitar Tel Aviv Bat Yam alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka Maccabi Tel Aviv, zote za Israel.
Kisoka, Miroshi aliibukia akademi ya Azam FC, kabla ya kutolewa kwa mkopo Biashara United akapate uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ambako msimu wake wa kwanza tu alipata nafasi ya kwenda Israel.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post
Alert: Content is protected !!