Na mwandishi wetu Dar-es-Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeendea kushikilia msimamo wake wa kumshinikiza Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kuwatimua bungeni wabunge 19 wa viti maalum.
Wamesema kuwa kitendo Cha Spika kuendelea kuwavumilia wabunge hao kuhudhuria vikao vya bunge Ni kitendo haramu na uvunjaji wa katiba
Kauli hiyo imetolewa leo Jumapili Juni 26, 2022 na Spika wa Bunge la wananchi la chama hicho, Celestine Simba alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar-es-Salaam.
Amesema Chadema haijapokea wito wala taarifa yoyote kutoka mahakamani kuhusu kufunguliwa kwa zuio au kesi mpya inayowapa haki wanachama hao kubaki bungeni.
"Kuhusu uamuzi wa mahakama wa Juni 22, 2022 tayari tumeshapokea nakala ya hukumu na tumeiwasikisha Tume ya Taifa ta Uchaguzi (NEC) na Bungeni kusisitiza kuondolewa kwa wabunge hao haramu," amesema Celestine.
Pia, kimeishauri CCM kukaa mezani na Spika Dk Tulia kwa kile walichodai 'kumpa somo' kiongozi huyo wa Bunge namna ya kukiongoza chombo hicho.
Juni 22, 2022 Mahakama Kuu ilitupilia mbali zuio la wabunge hao baada ya hoja mbili kati ya sita za pingamizi zilizowasilishwa na Chadema kubaini dosari za kisheria katika zuio hilo.